Kila mtu huwa anajiuliza ni jinsi gani ya kuondoa mafuta tumboni, iwe
tumbo ni la kati au ni kitambi kimejitokeza. Kwa mwili mnene wenye
mafuta mengi ni vigumu kuona matokeo mazuri ya kuridhisha kwa kufanya
mazoezi pekee, maana asilimia hamsini ya mafuta mwilini huifadhiwa chini
ya ngozi, na kiasi kingine kilicho baki huwa ndani ya misuli. Kufanya
mazoezi ya mwili pekee hakuwezi kuondoa mafuta hayo mwilini.
Mtu mnene akifanya mazoezi ya kuvuta tumbo hawezi kuona matokeo, hata kama akirudia mazoezi hayo mara mamia kwa siku, kitakachotokea ni kweli ataimalisha misuli yake ya tumbo ila hatoweza kuona matokeo hayo kwa sababu tumbo bado litakuwa limezungukwa na mafuta.
JINSI YA KUPUNGUZA MAFUTA
Kuna usemi unaosema, kwa matokeo ya mazoezi unahitaji.. “ASILIMIA 70 DAYATI, ASILIMIA 30 ZOEZI!”. Kwa matokeo mazuri na ya haraka njia hii hutoa matokeo mazuri Zaidi tofauti na kupiga mazoezi pekee ambapo ni kweli unaweza kuwa unaumguza mafuta mwilini ila hauwezi kuunguza mafuta yakutosheleza kwa siku kuweza kuonyesha matokeo mazuri ya mazoezi unayopiga.
Ila kwa njia ambayo itakupa matokeo ya muda mrefu maara nyingi huwa ni ya kufanya mazoezi kwa muda mrefu, na matokeo haya nayaita ya muda mrefu maana mazoezi hayo yatakufanya uwe na adabu ya kubadilisha mwenendo wa maisha yako na kuutunza mwili wako kwa heshima.
Njia ya 70 kwa 30 inatoa matokeo mazuri maana asilimia 70 ya upunguaji wa mafuta mwilini hufanywa na dayati ya kuangalia nini cha kula na kipi cha kuondoa kabisa kwenye mlo wako wa kila siku. Hata hivyo kwa kuangalia dayati pekee haiwezi kukupa matokeo mazuri, maana tafiti mbali mbali za kisayansi juu ya kupunguza mafuta mwilini zimeonyesha huwezi kupunguza mafuta mwilini kwa dayati pekee na kupata mwili wa kuvutia pasipo kufanya aina yeyote ya mazoezi ya mwili, ukitaka mwili uliopungua kwa mpangilio na mvuto lazima uhusishe pia mazoezi ya mwili.
Njia kuu ya kupunguza mafuta kwa njia ya dayati ni kupangilia milo yako ya siku.
Lazima ujue mlo wako utaupangilia katika hali gani, kwa mfano badala ya kula ovyo hovyo, unatakiwa upangilie milo yako kwa kula kiasi, kama umezoea kujaza tumbo wakati wa kula, jaribu kushusha mlo wako uwe unakula kwa kuondoa njaa kwa kuupa mwili vile virutubisho unavyovihitaji tu, na unaweza kula milo mitatu mpaka mitano kwa siku na usizidishe zaidi ya hapo.
Hakikisha unakula mlo kamili ila kwa kuhakikisha huli vyakula vilivyotengenezwa kwa sukari, na zingatia kuachana na milo inayotayarishwa kwa haraka, (fast sood) kama chipsi, vitafunwa na vinginevyo vinavyohusiana na hivyo, zingatia kula vyakula vyenye protini na milo yako iwe kamili na hasa pendelea kula mboga mboga.
Kwa kuzingatia dayati na kwa kufanya mazoezi yanayohusisha kuchemsha mwili wako kwa kuongeza mapigo ya moyo zaidi utafanya mwili wako ubadilike na kupata matokeo unayo yahitaji, maana kwa kadri mwili wako unavyochemka ndivyo unavyozidi kuchoma mafuta mwilini, na kwa jinsi mwili wako unavyopunguza mafuta utafanya ngozi yako kukakamaa na kufanya mwili wako kupata shepu, kwa hiyo kitu cha kufanya ni kukazania mazoezi yanayoongeza mapigo ya moyo na kusababisha upumuaji wa haraka, fanya mazoezi hayo mara tano kwa wiki.
Mazoezi yote unayofanya hakikisha yanahusisha sehemu zote za mwili kuanzia misuli ya mikono, nyonga, mgongo, mapaja, misuli ya chini ya miguu na sehemu zote za mwili kwa ujumla.

No comments:
Post a Comment