Ni
jambo la kawaida kujiuliza kama unampenda Fulani au kama Fulani
anakupenda. Katika tafakari hii, wengi hujikuta wakipata tafakari
tofauti.
Uzoefu
wangu unanifanya niamini kuna maana tofauti kuu 3 zinazojitokeza
miongoni mwetu wakati wa kutafakari swala la upendo katika mapenzi.
Jiunge nami katika tafakari hii kwa kusoma jinsi watu wanavyotafsiri tofauti neno Upendo katika mahusiano:’-
1.Kujali:
Kuna
wanaoamini kuwa kujali tuu inatosha kuonyesha kuwa unampenda fulani, au
fulani kuonyesha anakujali basi hiyo ndio maana halisi ya upendo. Wengi
hujikuta wakitumia muda mwingi kutafuta zawadi na surprises za ‘nguvu’
kama sehemu kuu ya kuonyesha upendo wao. Aina hii ya upendo inahusika
sana hasa kwa watu waliopo mashuleni na vyuoni. Wengi wanaoamini maana
hii ya upendo, husisitiza sana kuogopwa/kunyenyekewa kama sehemu ya
kuonyeshwa kuwa nao wanapendwa.
2. Kujitoa kafara:
Katika
maana hii, upendo ni swala la jinsi gani unavyojitoa kwa mwingine ili
kuona anakuwa na furaha na ajihisi kuwa salama kutokana na uwepo wako.
La msingi katika aina hii ya upendo ni kupenda kumfahamu vema mwenzi
wako, kujua shida zake, na ndoto zake, na kujitoa kwa hali na mali
kuhakikisha anaona uwepesi katika shida zake, na kuwa anakuwa na
matumaini ya kuwa ndoto zake zitatimia. Upendo wa namna hii huwa na
subira, na huonekana zaidi kwa waliokomaa kifikra, na wenye kujiheshimu
wao wenyewe.
3.Kuvutia:
Kwa wengine upendo ni namna gani wanavyovutiwa kimapenzi na mtu husika, au vile wanavyojisikia kuwa salama mbele ya mtu fulani. Utakuta
mtu anasema anampenda kaka fulani kwakuwa tuu amevutiwa na uhodari wa
kijana husika katika masomo, kujiheshimu kwa kijana husika, sifa au
umaarufu alionao mhusika. Na kwa upande mwingine, mtu anaweza kuvutia
kwa uzuri wa sura au umbile la mtu fulani. Kutokana na mvuto wa hisia
kama hizo na wakati mwingine hisia hizi za mvuto huwa kali sana, basi
mtu akadhani hiyo ndiyo maana halisi ya Upendo. Wenye tafakari hii ya
upendo wengi wao hawana subira na ukichukua muda mrefu kutafakari hisia
hizi, unaweza kukuta ni za muda mfupi tuu.
Hitimisho:
Pamoja
na ukweli kuwa mvuto wa kimapenzi kwa mtu unayejenga nae mahusiano ni
muhimu. Na kwamba kujaliana na kunyenyekeana ni vigezo muhimu katika
kujenga mahusiano yenye furaha, mambo hayo pekee hayatoshi kusema kuna
upendo. Upendo ni jambo lisilo na ubinafsi, haliangii nafsi yako inataka
kunufaika kiasi gani, bali unataka kuinufaisha nafsi ya mwingine kwa
kiwango gani. Hivyo kwa upande wetu, maana ya upendo tunayoipendekeza ni
Kujitoa Kafara, kama tulivyoielezea hapo juu.
No comments:
Post a Comment