Artikel Terbaru

Responsive Ads Here

Monday, April 23, 2018

NAHISI MUME WANGU ANA NISALITI,..JE NIFANYAJE??..NAOMBA USHAURI PLEASE!


Nilikuwa siangalii simu ya mume wangu kipindi chote tumeoana ila nilipoona anakuwa busy sana na simu nikahisi kuna walakini. mnatoka out busy chating mnakula mnamaliza busy na simu. mkirudi nyumbani busy na simu anaweka simu saa ya kwenda kulala tu. hamuwezi discuss mambo ya maana.

maumivu makali. nilijua labda anachat na marafiki niliposhika simu yake nikaingia facebook yake niliyoyakuta ni masikitiko, anachat na wanawake wanaambizana wakikutana watafanya nini, wanamke anaandika mpaka nahamu ya kufanya mapenzi na wewe toka tu sex kwenye simu.

wanatumiana picha za uchi na kuonyesha matiti, anawaambia yeye kwenye game yupo safi watafurahia. kafungua account fake facebook hatumii jina lake ambayo ndio kuna upuuzi wote ndani ila kwenye simu ukifungua tu unaona.

fikiria umekaa na mume wako unajichekesha, unampikia, unasema wapi tatizo mbona yupo busy kumbe yupo busy na wanawake wengine anachat nao. wengine anawatumia nauli toka arusha waje dar ina maana anatembea nao waje kufanya nini?

sijamwambia lolote sijui nianzie wapi ila kuna wanaonipenda wengi nje nawaza nimlipizie? hatujajaliwa kupata mtoto hata mmoja bado ila kwa idadi hii ya wanawake kwenye simu yake sioni muelekeo mbele tutaishia kutafuta hela yeye atatuma nauli waje wamfurahishe. nimeona mengi siwezi muamini tena na mahusiano yangu ya zamani x-boyfriend wangu alikuwa na tabia hizi na hakuziacha ni bora niachane nae niishi kama wema sepetu au jlo kuliko kukaa na wanaume mbwa.

naumia muda huu ningeutumia kuwaza mambo ya maendeleo, tukikaa tungeongea mipango ya maisha, kutaniana na kujenga urafiki zaidi kati yetu naona natumia nguvu nyingi kwa kujenga penzi. mbaya zaidi katika swala la kufanya mapenzi mpaka mimi nianze yeye hanishiki hata siku moja labda hana mapenzi tena nami.

No comments:

Post a Comment