Hello reader wa N.M blog,
Wakumbuka wakati ambapo tulikuwa watoto wadogo?
Kabla hujaenda kulala, ulikuwa ukifuata tabia ambayo ilikuwa lazima uitimize.
Wengine wetu walikuwa wakiangalia kwa makabati...
Wengine wetu walikuwa wakiangalia chini ya kitanda...
Wengine wetu walilala taa ya usiku ikiwa wazi...
Wengine wetu walikuwa wakiwauliza wazazi iwapo "zimwi mtu"(boogey man) atakuja kuwachukua usiku huo.
Tulikuwa na kipawa kikubwa cha kuwa na mawazo katika fikra zetu.
Fikra zetu zilikuwa za nguvu, nzito, na za ubunifu, ambazo zilitufanya tujenga dhana za majini ambayo hayakuwepo.
So huyo mtoto asiyekuwa na hatia alienda wapi? Well, huyo mtoto alikuwa
mkubwa na kusahau kuhusu "zimwi mtu" kwa sababu ilifika mahali akaanza
kufikiria kudeti wanawake.
Na pindi tu alipoanza kudeti wanawake, huyu "zimwi mtu" aliruka na
kuingia katika kichwa chake na kuanza kuishi katika akili yake.
Huu ndio ukweli mtupu.
Wanaume wengi mpaka sasa wanaishi na "zimwi mtu" katika vichwa vyao.
Hebu fikiria uoga unaokuwa nao wakati inapokuja kukutana na wanawake.
Fikia uoga unaokuwa nao wakati unapo approach mwanamke kwa mara ile ya
kwanza kabisa, na fikra ambazo zinakuzuia wewe kuongea na mwanamke kama
huyu.
Hizo fikra unazokuwa nazo wakati huo huwa ni huyo zimwi mtu. Huwa ni
toleo la zimwi mtu wa ukubwani. Na kwa bahati mbaya ni kuwa watu wakubwa
huwa na woga zaidi kuwaliko watoto wadogo.
Watoto wadogo huogopa vitu ambavyo havipo, na mpaka ile siku
watakapoumizwa wakifanya jambo flani, wataendelea kulirudia jambo hilo
mara kwa mara.
Wakati ulipokuwa mtoto mdogo ni mara ngapi ulikuwa ukicheza na kisu
mpaka ile siku ulipogundua ya kuwa kujikata kidole chako haikuwa jambo
zuri?
Lakini kama mtu mkubwa, ni mara ngapi ushawahi kuapproach mwanamke
mrembo na akakukataa halafu ukakubali zimwi mtu aingie na kuitawala
akili yako?
Umekubali zimwi mtu achukue kontrol katika akili yako.
Umejijengea zimwi mtu ambaye anakuwa na nguvu kuliko zimwi mtu yeyote yule ambaye ushawahi kumtengeneza katika fikra zako.
So tutafanyaje mpaka tumwondoe huyu jinamizi?
Tutafanyaje mpaka tuondoe huu uoga wa kuapproach wanawake?
Ni rahisi sana, tunaweza kukupatia motisha na uhakiki ambao unaweza
kuurudia mara kwa mara mpaka ukuige. Lakini kiukweli ni kuwa zimwi mtu
hajulikani wakati ambao anaweza kujitokeza.
Anaweza kuja wakati unaaproach mwanamke, wakati unapoongea, wakati mko deti ama labda kabla ya kufanya mapenzi.
So itategemea na vile ambavyo utajipanga wewe kwa sababu hapa Nesi
Mapenzi tumehakikisha ya kuwa tunautoa woga wowote ambao unaweza
kukabiliwa wakati unapotangamana na wanawake. Soma chapisho la jinsi ya kutoa uoga kwa mwanamke plus usome machapisho mengine ambayo yameandikwa spesheli ya kukabiliana na tatizo la kuapproach.
Sunday, April 29, 2018
'Zimwi Mtu' Ambaye Anawakabili Wanaume
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment