kuna watu wamekua wakiuliza mara kwa mara kama inaruhusiwa kushiriki
tendo la ndoa mpaka umri gani wa mimba au ni sahihi kufanya tendo la
ndoa kipindi cha ujauzito? maswali yalikua mengi sana hivyo leo nimeamua
nijibu maswali hayo na makala hii.
mwanamke akiwa na mimba anaruhusiwa kushiriki tendo la ndoa hata kama
anatarajia kuzaa kesho yake, hakuna tatizo lolote linalomzuia kufanya
hivyo, baadhi ya wanawake wamekua wazito sana kufanya hivyo kwa kua na
sababu mbalimbali za kujitetea bila kujua kwamba wanazikosa faida hizi
ambazo ni muhumu kiafya.faida zenyewe ni kama zifuatazo
husaidia uchungu mzuri na kupona mapema; kufika kileleni wakati
wa tendo la ndoa huambatana na kubana kwa misuli ya nyonga hii husaidia
kuweka imara misuli ya nyonga ambayo ni muhimu sana wakati wa kusukuma
mtoto na baada ya kuzaa kwani misuli hii ikiwa legevu mwanamke huweza
kushindwa kuzaa kwa njia ya kawaida na hata baada ya kuzaa huweza
kushindwa kuzuia mkojo usitoke wenyewe au kuvuja damu kwa muda mrefu.
hupunguza kwenda ovyo kukojoa au kujikojolea; wakati wa ujauzito
mtoto anapozidi kua mkubwa anazidi kukandamiza kibovu cha mkojo, hii
humfanya mama aende chooni kukojoa mara kwa mara na wakati mwingine hata
akipiga chafya au kukohoa basi mkojo unaweza kutoka wenyewe. tendo la
ndoa huibana misuli ya nyonga na kuzuia hali hii.
huzuia uwezekano wa kupata kifafa cha mimba; tafiti zinaonyesha
kwamba aina ya protini inayopatikana kwenye mbegu za mwanaume huongeza
kinga ya mwili na kuzuia uwezekano wa kupata kifafa cha mimba ambacho
kinaua wanawake wengi sana.
hutibu tatizo la kufika kileleni kwa shida; kipindi cha ujauzito
chuchu za mwanamke na kinembe chake huvimba na kuongezeka hisia mara
dufu huku kiwango cha homoni za oestrogen kikiwa juu sana, hii humfanya
kufika kileleni kirahisi sana kuliko mwanzoni.
huwapa uwezo wa kujiamini; kipindi cha ujauzito mwanamke hua
anapata hofu sana na kutojiamini na mwili wake, hua na wasiwasi kwamba
mwili wake unaharibika hivyo kitendo cha mwanaume wake kuendelea
kushiriki naye tendo la ndoa humpa kujiamini kwamba mwili wake bado uko
kwenye hali nzuri na anapendwa.
hupunguza msongo wa mawazo; kipindi cha ujauzito wanawake wengi
huwaza sana kuhusu kesho yao...je swala la uchumi litakuaje? mwili wangu
utakuaje? je ntapata jinsia nayotegemea? na kadhalika.. tendo la ndoa
hutoa homoni ya upendo kwa jina la oxytocin, homoni hii hupunguza mawazo
na kumpa amani mjamzito.
huongeza upendo na mshikamano kati ya wapenzi; katika hali ya
kawaida wanandoa wakikwazana wanaweza wakapatana kwa kushiriki tendo la
ndoa tu, amani na upendo kipindi hiki ni muhimu sana kwani kuna mtoto
anakuja ambaye anatakiwa kuzaliwa huku baba na mama wakiwa wanapatana.
hukuandaa na uchungu; ukishiriki ndoa wakati wa tarehe
zilizokadiriwa zimefika unapata homoni moja kutoka kwenye mbegu za
mwanaume kwa jina la prostglandin, homoni hii huivisha mlango wa uzazi
na kuanza kufunguka taratibu kujiandaa na uchungu.
hutibu tatizo la kukosa usingizi; wanawake wengi wajawazito hua
na dalili mbalimbali za maumivu na kuumwa sehemu tofauti za mwili na
msongo wa mawazo, hii huweza kuwakosesha usingizi kabisa..tendo la ndoa
huweza kuwapa usingizi mzuri.
hupunguza presha ya damu; kipindi cha tendo la ndoa presha ya
damu hushuka kwenye kiwango kizuri sana, hii ni muhimu sana kwa wanawake
wenye hatari ya kupata kifafa cha mimba kama wanene sana, wenye
kisukari au wenye historia za ugonjwa wa presha kwenye koo zao.
mwisho; hakikisha unatumia staili za tendo la ndoa ambazo
hazimuumizi mtoto na mama yaani hakikisha haulilalii tumbo hasa mimba
ikiwa kubwa, kuna staili muhimu kipindi hiki kama kuangalia upande
mmoja, mwanamke kuja juu, au mwanamke kuinama
No comments:
Post a Comment