wengine hujifunika mashuka au blenketi. Kwa mujiu wa makala mbalimbali za afya zinaeleza kuwa si vizuri kiafya kulala na nguo.
Hizi ni faida chache za kuto lala na nguo nyakati za usiku.
1. Hutengeneza uhusiano mzuri ukisaidiwa na kichocheo cha Oxytocin.
Natasha Turner, daktari wa tiba asilia aliyeandika kwenye blogu ya Huff
Post Canada, alifichua kwamba kulala karibu au mkiwa mmekumbatiana na
mwenzi wako mkiwa bila nguo hufanya mwili kutoa kichocheo kiitwacho
Oxytocin kinachofanya ujisikie vizuri. Hii inatokea pale kunapokuwa na
mgusano wa ngozi kwa ngozi, hii inaweza kusaidia kuondoa msongo (Stress)
na kushuka moyo (Depression). Oxytocin pia inaweza kupunguza shinikizo
la damu, kuimarisha tumbo na kupunguza uvimbe kwenye utumbo. Pia,
utendaji wako wa tendo la ndoa pengine unaweza kuboreka.
2. Hukufanya ubaki kijana.
Inashauri kuweka mwili katika jotoridi chini ya 21°C ukiwa kitandani na
njia nzuri kufanta hivyo ni kulala uchi/mtupu. Hii huruhusu vichocheo
vinavyozuia uzee na Melatonin ambayo hudhibiti mzunguko wa kusinzia na
kuamka kutenda kazi vizuri. Utajihisi huru, Kulala kitandani kwako, bila
kuvaa chochote inakufanya kujisikia huru.
3. Huhamasisha vichocheo vya furaha.
Unapolala na nguo au kulala chini ya blanketi zito unazuia utokaji wa
kichocheo cha ukuaji (Growth Hormone/HGH). Hii ina maana hutoweza
kupunguza mafuta ukiwa katika usingizi au hautofaidika na ukarabati wa
usiku wa mifupa, ngozi na nyama za mwili wako.
Kulala uchi/mtupu pia huthibiti kiwango cha Cortisol, zinazo dhoofisha
kinga ya mwili, kupandisha shinikizo la damu na lehemu (Cholestrol),
kuvuruga mpangilio wa usingizi, kupunguza hamu ya tendo la ndoa na
kuongeza hamu ya sukari.
4. Inatunza afya viungo vya uzazi.
Kina dada, mnafahamu mnaweza kupunguza matatizo ya mabukizi ya fangasi
kwa kulala uchi/watupu? Unaweza kupunguza kuzaliana kwa fangasi na uke
wako utakushukuru kwa hilo. Vilevile wanaume wanaweza kufaidika kulala
uchi/watupu kwa kuwa korodani zinakuwa katika jotoridi la kutosha na
uzazi unaongezeka.
5. Mzunguko wa damu unakuwa bora
Hakuna kitu kibaya kama lastiki inayozuia mzunguko wa damu. Ondoa nguo
zenye lastiki na utajipata uko na furaha kwa mtiririko wa damu mzuri
ndani mwili wako, vile vile inaelezwa kuwa ukiwa hauna nguo inasiaia
kutunza ngozi yako kwani inaweza kupumua vizuri.
6. Kutokuwa mvivu
Faida nyingine ni kwamba mara baada ya kuamka unakuwa na ulazima wa
kuvaa nguo kwa ajili ya siku hiyo mpya na sio kuamka na nguo zako za
kulalia na kutoka nazo nje.
Chanzo Mtandao
Tuesday, June 12, 2018
Faida za Kulala Bila Nguo Nyakati za Usiku
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment