Wataalamu wa magonjwa ya mfumo wa uzazi wameeleza kuwa tabia ya kupenda
ngono kupitia kiasi ni ugonjwa wa akili ujulikanao kwa jina la ‘mania’
(sexual disorder).
Akizungumza na Mwananchi, daktari bingwa wa magonjwa ya kinamama na
uzazi kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Colman Living amesema
kufanya ngono mara kwa mara huimarisha ubongo lakini kupita kiasi
husababisha madhara mbalimbali kwa mwili.
“Kiafya kuna madhara ikiwemo maambukizi ya magonjwa kama yapo sambamba
na kukinai tendo, lakini hapohapo kuna mwingine anakuwa na hulka ya
kupenda tendo hilo kwa sababu ni mgonjwa tunaita ‘sexual disorder’ au
kitaalamu unaitwa ‘mania’ huu ni ugonjwa wa akili kwamba yeye anakuwa
hatosheki hivyo anafanya mara kwa mara na wakati mwingine na watu
tofauti,” alisema Dk Colman.
Akielezea madhara kwa wanawake, Dk Colman alisema kwa anayependa tendo
hilo licha ya kuchanika sehemu za siri, inategemea anafanya na watu
wangapi, kama ni tofauti anaweza kupata magonjwa mbalimbali.
Alisema kufanya tendo la ngono sana humfanya mwanamke kuwa katika hatari
kubwa ya kupata mimba zisizotarajiwa ambazo wakati mwingine zinaweza
kuambatana na kifafa cha mimba, kuathirika kiuchumi sababu mama atakuwa
na watoto wengi ambao hawezi kuwapa mahitaji ya muhimu ikiwemo elimu,
chakula na matibabu.
“Kwa wanawake saratani za njia ya uke huwaathiri zaidi hasa ile ya
shingo ya kizazi ambayo kwa ujumla wake karibu asilimia 90 ya aina hizi
za saratani husababishwa na virusi vya HPV ambavyo huambukizwa au
kuenezwa kwa njia ya ngono kama ambavyo anapata maradhi mengine kama
Hepatitis B, HIV na mengine yasababishwayo na ngono zembe,” alisema Dk
Colman.
Hata hivyo alifafanua kuwa ngono kupita kiasi husababisha maambukizi
mengi katika njia mbalimbali za mwili zilizowazi kama mdomoni, kwenye
uke na sehemu ya haja kubwa.
Akizungumzia hilo Mkurugenzi wa Manundu Dispensary iliyopo Korogwe, Dk
Ally Nzige amesema ikiwa mwanaume atafanya ngono mara kwa mara inamweka
katika nafasi kubwa ya kuepukana na magonjwa mbalimbali yasiyoambukiza,
lakini asipitilize kiwango na kubadilisha wapenzi.
Alisema kwa kawaida mtu anatakiwa kufanya tendo la ngono angalau mara tatu kwa wiki ni kiwango kizuri kwa afya.
“Umri sahihi kwa mwanaume kuanza kuwa tayari kwa tendo ni miaka 18 mpaka
35, hapa tunategemea kwamba awe ameshafanikiwa hata kupata watoto
vinginevyo na hapo huyo atakuwa na matatizo ikiwa hatataka kujihusisha
na tendo hilo hasa baada ya miaka 22,” amesema.
Dk Nzige amesema mwanaume anapokwenda zaidi ni kitu ambacho hakina shida ila inategemea na huyo patna amekubali au anamkomoa.
“Lakini hii inamtaka mtu mwenye afya iliyokuwa nzuri, pamoja na hayo
inasaidia mtu kutulia kwa wale ambao wapo kwenye ndoa pia hawa
wanachelewa kupata matatizo mengi, lakini watu ambao hawajaoa wala
kuolewa wanapata magonjwa mbalimbali ya msongo wa mawazo, lakini ni
suala la msingi kuwa na utulivu katika ndoa kwani kama huna ratiba nzuri
ya maisha vitu vingine vitakushinda,” amesema Dk Nzige.
Hata hivyo amesema hakuna madhara kwa mwanaume kufanya tendo la ndoa
kupita kiasi, lakini iwapo atafanya na watu tofauti anaweza kupata
maradhi mbalimbali yanayoambukizwa kwa njia ya ngono.
Saturday, June 9, 2018
Home
/
Unlabelled
/
Je Wafahamu Kuwa Kupenda Ngono Kupita Kiasi ni Ugonjwa wa Akili (Sexual Disorder)?
Je Wafahamu Kuwa Kupenda Ngono Kupita Kiasi ni Ugonjwa wa Akili (Sexual Disorder)?
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment