Naandika nikiwa na kilio cha jitimai na majonzi yasiyoisha milele.
Mwezi desemba mwaka jana nimefunga ndoa na mke wangu.
Lakini tangu tufunge ndoa nikawa na mashaka na mwenendo wa mke wangu.
Wiki mbili zilizopita nilipata jambo la ajabu. Mke wangu kaniambukiza
ugonjwa wa ngono. Nilipomuuliza akadai kuwa hajui amepataje.
Nikimweleza twende hospitali anakataa. Nimeenda nikatibiwa na naendelea na tiba.
Juzi usiku nikiwa nataka kupata ukweli nikaja nyumbani na kumwomba
tuongee chumbani. Nikatumia mbinu ya kijeshi nikatoa bastola yangu
ambayo hajawahi kuiona hata siku moja na nikaanza kumsaili.
Mke wangu akanitajia orodha ya wanaume aliotembea nao ktk kipindi hichi
cha ndoa ya miezi 5 inatisha. Katembea na wanaume sita tofauti.
Nilijikuta napoteza nguvu na fahamu. Nilipozinduka mke wangu kadai tutengane kwani dhambi aliyonitendea haipaswi kumsamehe.
Kila baada ya kama masaa 3 napoteza fahamu. Ndugu zangu hawana taarifa.
Lakini ndugu na wazazi wa mwanamke wanajua kinachoendelea.
Ni ngumu kuamini ktk hali ya kawaida lakini najikuta kila akija mwanamke
akija kunijulia hali nataka kuzimia tu na napata hasira.
Sitofika kupenda tena na nawachukia wanawake hata mama yangu mzazi aliyenizaa.
Monday, June 18, 2018
KWA Hili Nitawachukia Wanawake Milele...Na Sitowasamehe
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment