Wadau hamjambo,
Naomba msaada, niko South Africa since last week, niliondoka Tz mpaka
South Africa baada ya kupata mchongo kwa rafiki yangu ambaye
alinitafutia mchongo wa kazi.
Namshukuru Mungu nilifika salama na maisha yanaendelea vyema kabisa.
suala kubwa lililopo ni kuhusu wife wangu, kipindi naondoka
nilimshirikisha lakini alionekana kuwa na hasira sana juu ya uamuzi
wangu wakuja South,
Nilijaribu sana kumsihi yakuwa nakuja kuangalia namna mambo au upepo
ulivyo kisha nitageuza lakini alishindwa kunielewepa kabisa na kuwa mtu
mwenye hasira kiasi ambacho hata unyumba alininyima.
Nikafikiri sana namna gani yakufanya, sikuona namna, maana nilikuwa
tayari nishakatiwa ticket ya kuja na kurudi(Go and Return) yaani kama
mambo yakiwa mabaya niko huru kurudi. Basi kiukweli nilichukua uamuzi
mgumu nikafwatilia kila kitu na safari ikaiva yakuja South, nikaondoka
na kufika salama.
Lakini kabla sijaondoka wife alinitumia sms na kuniambia nisimshirikishe lolote wala kumpigia wala kuhangaika na yeye.
Sasa tangu nimefika nimejaribu kumtumia sms, kutaka kujua hali ya
maendeleo na nilimwomba hata akaunt ya bank ili nimtumie pesa kwa ajili
ya matumizi, lakini wadau huyu mwanamke alinitukana na kunitumia sms za
ajabu sana, oooh, wewe mwanaume gani, tena kwa taarifa yako nimeshapata
baba wa mtoto na maneno mengine mengi ya ajabu.
Kweli najisikia vibaya sana na majuto kuwa na mwanamke mwenye hasira na
asiye na kipimo cha maneno kwangu kwa heshima. Japo alinitukana vya
kutosha lakini sijaacha kumtumia sms za kutaka kujua hali yake na mtoto,
ila cha ajabu hajibu chochote.
Niko njiapanda, nishaurini nifanye nini, kwa wadau naombeni ushauri
wenye hekima ili niuchukue maana niko mbali na ninahisi kuumia sana.
Please ushauri sio kejeli.
Thanks wadau.
Nawasilisha
Saturday, June 9, 2018
Nahitaji Ushauri, Mke Amebadilika Sana Tangu Mimi Niondoke..
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment