HII ni hali ambayo mwanamke anakuwa na hamu ya kufanya tendo la ndoa lakini anapata ugumu kutokana na maumivu makali anayopata.
Hali hii inatokana na kubana au kukaza kwa misuli ya uke lakini pia inaweza kusababishwa na matatizo ukeni.
Mfano endapo kuna michubuko au vidonda au kasoro yoyote ya uke, aidha
uke ni mdogo au maumbile ya uke hayana uwiano na uume. Tatizo hili
huwapata wanawake wa rika zote ilimradi tayari yupo katika umri wa
kuzaa.
TATIZO LINAVYOGAWANYIKA
Tatizo hili la maumivu wakati wa tendo la ndoa limegawanyika katika maeneo makuu mawili. Kwanza ni Primary Dyspareunia .
Hapa mwanamke anakuwa hana historia ya maumivu wala hana historia ya
kuwahi kufanya tendo hilo ndiyo, kwanza anaanza. Kitaalamu hali hii ya
maumivu huitwa Honey moon Dypareunia au maumivu ya fungate na hutokea
mara tu anapoanza kujamiiana kwa mara ya kwanza. Katika hali hii misuli
ya uke inaweza kubana kutokana na michubuko au kuchanika ubikira au hata
kuchanika upande wa chini wa uke na wakati mwingine michubuko hutokea
katika tundu ya mkojo.Hali ya michubuko inaweza kuwa mbaya na
ikajitokeza hata kwa kugusa tu upande wa nje wa uke.
Maumivu yakiendelea au yakizidi husababisha mgonjwa apate matatizo ya
kisaikolojia kiasi kwamba huanza kuogopa tendo lenyewe na kuhisi endapo
atalifanya ataumia. Tatizo hili likileta michubuko kwenye njia ya mkojo
husababisha maambukizi sugu ya kibofu cha mkojo kutokana na michubuko ya
mara kwa mara ya tundu ya mkojo.
Maumivu ukeni hutokana pia na maandalizi mabovu kabla ya tendo ambapo
uke unakuwa haujalainika kwa kutofanya romance ya kutosha, kutofanya
tendo hilo kwa ustaarabu, yaani kutumia nguvu au endapo mwanamke atakuwa
na maambukizi ukeni mfano fangasi ambayo huambatana na kutokwa na
uchafu ukeni na muwasho, magonjwa ya uke kama kuvimba kwa tezi za uke,
kuvimba kwa mashavu ya uke au hali yoyote inayomwondolea amani mwanamke
pale ukeni inaweza kumfanya kisaikolojia aathirike na kuhisi maumivu
wakati wa tendo.
Michubuko ukeni au kuhisi moto ukeni wakati wa tendo la ndoa kunaweza
kusababishwa na matumizi ya vilainishi visivyofaa au kuumwa kutokana na
uwepo wa vinyweleo virefu ukeni na endapo havikupunguzwa vitaingia
ukeni wakati wa tendo na kukuchubua. Kasoro katika ubikira pia
husababisha mwanamke ahisi maumivu wakati wa tendo.
Maumivu haya huwa hayahusiani na yale ya awali ya fungate na wakati
mwingine huanza baada ya kipindi kirefu cha miaka mingi tangu uanze
tendo la ndoa na wengine huwa na tatizo hili tayari wana watoto. Chanzo
cha tatizo hili ni ukavu ukeni, umri mkubwa wa mwanamke na kusinyaa kwa
misuli ya uke.
Matatizo haya isipokuwa la umri mkubwa hutokea katika umri wa kati na
tayari mwanamke anayo historia ya kuwa katika mahusiano na hata tayari
ana watoto. Umri mkubwa tunaouzungumzia ni zaidi ya miaka hamsini.
Kubana misuli ya ukeni hutokana na makovu baada ya kushonwa msamba au
kuongezewa njia wakati wa kujifungua au upasuaji wa kurekebisha fistula
pia husababisha tatizo hili.
Vyanzo vingine vya maumivu haya ya tendo la ndoa ni kushuka kwa kizazi
ambapo mwanamke atahisi kitu kama gololi ukeni wakati akijisafi sha au
kuhisi kizazi kinasukumwa wakati wa tendo, kugeuka kwa kizazi, matatizo
katika tabaka la ndani la kizazi, maambukizi sugu ukeni ambapo uchafu na
muwasho ukeni hujirudiarudia, matatizo katika njia ya mkojo na
maambukizi katika viungo vya uzazi ’PID’ husababisha maumivu wakati wa
tendo la ndoa.
Matitizo ya kisaikolojia husababisha maumivu wakati wa tendo la ndoa
pale ambapo misuli ya ukeni itakaza na mwanamke anapochunguzwa huwa hana
tatizo au kasoro yoyote ukeni. Matatizo katika mishipa ya fahamu ya
ukeni, kuogopa tendo lenyewe kuhisi utapata maumivu au kama kuna
historia ya kuingiliwa kwa nguvu na ukaumia, kutokuwa na taarifa sahihi
kuhusu tendo la kujamiiana, yote haya na mengine mengi humharibu
mwanamke kisaikolojia na kujikuta anaanza kuhisi maumivu hata kabla ya
tendo lenyewe kwa kuingiwa na hofu.
Hali nyingine inayoweza kumfanya mwanamke aathirike kisaikolojia na
asiwe tayari kwa tendo na hata akilifanya apate maumivu ni kuogopa
kupata ujauzito wakati hayupo tayari kwa hilo, kuogopa kupata
maambukizi, kulazimishwa penzi endapo haupo tayari na mwanaume uliye
naye na kuhisi kuna tofauti ya maumbile na mume uliyenaye.
Endapo mwanaume anakukwaza kutokana na kutokwa na jasho jingi sana
wakati wa tendo, kutoa harufu mbaya ya pua, kinywani, makwapani au
sehemu zake za siri, huwa na magonjwa ya ngozi au hata mwilini mwake,
matatizo haya huweza kumwathiri mwanamke kisaikolojia na asifurahie
tendo na kutotoa ushirikiano wakati wa tendo na kupata maumivu.
UCHUNGUZI Tatizo hili ni pana sana, unaweza kuhisi una kasoro au
maambukizi kumbe tofauti. Kwa hiyo basi ni vizuri uchunguzwe kwa umakini
katika kliniki za madaktari wa akina mama katika hospitali za mikoa ili
kujua chanzo halisi cha tatizo.
No comments:
Post a Comment