Kuna watu wana Mikwara sana, ukiachana nae anaanza Maneno ya shombo,
wengine hudiriki kukwambia ''you cant live without me utarudi tu'',
unajiuliza huyu mtu ana Hisa kwenye mishipa yangu ya moyo au ana mrija
wa Oxygen yangu ya kutumia kesho?? Kama nilizaliwa peke yangu kwanini
nisiweze kuishi wewe ukiondoka??
Maneno ya mkosaji haya, usiyasikilize kamwe! Unapoamua kufanya Maamuzi
magumu usisikilize kingine chochote, Follow your heart. Wengi wamegeuzwa
watumwa kwa kuamini they cant live bila watu fulani, kisa wamezoeana,
au wamekaa muda mrefu kwenye mahusiano, unahisi kama hutaweza... Hamna
kitu kisichowezekana, Mungu ameumba kusahau, utapona maumivu na
utasonga! Hakuna destiny rahisi ya Kimapenzi bila kufanya maamuzi
magumu, lasivyo Jiandae kuwa mtumwa wa mtu fulani, binadamu fulani
ambaye naye amegundua wewe ni dhaifu na anatumia udhaifu wako kukutesa
maisha yote...
Amua leo, Uwe mtumwa wa mtu au utengeneze furaha yako kwa Kumove on kupata Lover of you life
Sunday, July 1, 2018
Unatamani Kumuacha ila Unashindwa? Ngoja Nikwambie Kitu
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment