Na Ahmad Mmow, Lindi.
Mwanamke anayetambulika kwa jina la Fatuma Abdurhaman,mkazi wa Kilwa
Kivinje anadhaniwa kutaka kumtupia chooni mtoto wake baada ya
kujifungua.
Kwamujibu wa maelezo ya mama mzazi wa Fatuma,Mwajuma Luwawi kitendo
hicho cha kikatili kimefanyika leo asubu.Hata hivyo mama huyo(Mwajuma)
aliwahi kumuokoa mtoto huyo kabla hatoswa chooni.
Mwajuma alisema alisikia kilio cha mtoto mchanga chooni,alipokwenda
alimkuta Fatuma huku kitoto hicho kikiwa chini karibu na shimo la
choo.Hivyo kulazimika kuomba msaada kwa majirani ambao walikwenda na
kufanikiwa kuwapeleka kichanga na mama huyo katili katika hospitali ya
wilaya Kilwa(Kinyonga).
Kwaupande wake Fatuma alipoulizwa akiwa katika hospitali hiyo ya
Kinyonga,kwanini alikwenda kujifungulia eneo lisilo sahihi,alisema
akikuwa hajui kama alikuwa na mimba.Japokuwa anamtoto wa mwenye umri wa
miaka mitatu.
Fatima katika utetezi wake alisema alipokuwa anakwenda hospitali akikuwa
anaambiwa ana vidonda vya tumbo na anadonge tumboni.Kwahiyo hata
alipokwenda chooni humo hakujua kama atajwenda kujifungua.
Fatuma alipoulizwa kama hakusikia uchungu kabla na wakati
wakujifungua,akisema akikuwa hajisikii uchungu wowote.Kutokana kutohisi
kama anamimba kulisababisha asiende kliniki katika kipindi chote cha
ujauzito wake.
Kwamujibu wa muuguzi wa zamu katika chumba cha wazazi,Fatuma na mtoto
huyo wa kike afya zao ni mzuri.Hatahivyo anaendelea kupata huduma za
msingi hospitalini hapo kabla hawajaruhusiwa kuondoka.
Alipoulizwa kamanda wa polisi wa mkoa wa Lindi,kamishina msaidizi wa
polisi,Pudensiana Protas kuhusu tukio hilo.Alisema hakuwa na
taarifa.Bali atafuatilia ilikujua ukweli wa tukio hilo.
Juhudi za kumpata mganga mkuu wa wilaya ya Kilwa hazikufanikiwa kutokana na mganga huyo kuwa nje ya ofisi.
No comments:
Post a Comment