Zoezi la kujifungua linafariji na kuchosha pia, ni la faraja sana kwa
kuwa linakufanya uwe mama? Wiki 4 za mwanzo kwa mzazi zinaweza kuwa
katika kumbukumbu zako kwa muda mrefu kwakuwa ni wiki za ‘majimaji’ tu –
jasho, kunyonyesha na haja ndogo kutoa majimaji yote ya ziada mwilini
mwako. Inashangaza hata kama mtu utakuwa na hamu ya kufanya mapenzi
katika kipindi hicho.
Madaktari wanasema kuwa mwili wa mwanamke unahitaji wiki 6 kurudi kwenye
hali yake ya kawaida. Katika kipindi hiki cha wiki 6, mfupa wa nyonga
na uti wa mgongo hurudi kwenye hali yake ya awali. Homoni zako pia
zinajirekebisha sambamba na misuli iliyopo kwenye sakafu ya nyonga
kupumzika wakati ikirudi kwenye hali yake iliyokuwa nayo mwanzo kabla ya
kazi kubwa iliyotoka kuifanya ya kumbeba mtoto na kusaidia kwenye
kumtoa wakati wa kujifungua.
Kwahiyo, mpaka kitakapofika kipindi hiki cha wiki 6, unashauriwa
kutofanya mapenzi, lakini haimaanishi kwamba huwezi kufanya mambo
mengine kama kumbusu, kumshikashika, au kumnyonya mwanaume wako, na yeye
kukufanyia hivyo hivyo. Wanawake wengine wanasema kuwa chuchu zao huwa
na hisia sana kutokana na kunyonyesha kiasi kwamba wanaweza kufika
kileleni kwa kushikwa chuchu tu.
Lakini kuhusu dawa za kuzuia kubeba mimba katika kipindi hiki,
mnashauriwa muwe na tahadhari kuhusu kutumia njia yoyote itayoathiri
mfumo wa homoni. Hii ni kwa sababu itaathiri sana kiwango na ubora wa
maziwa na itamsababishia mtoto kutopata lishe inayotakiwa. Pia, vidonge
vyenye oestrogen vimethibitishwa kusababisha kupungua kwa kiwango cha
maziwa kwa mama anayenyonyesha, na mara nyingine hupunguza ghafla sana.
Shirika la Afya Duniani linasisitiza mtoto anywe maziwa tu kwa muda
usiopungua miezi 6 kisha uendelee kumnyonyesha mpaka atakapofikisha
miaka miwili. Wazazi wengi wanaona hii inawatesa na wengi wao wanasema
kwamba miezi 6 ya mwanzo ni muhimu sana.
Unashauriwa uzungumze na daktari wako kuhusu muda gani unaweza kurudia
kufanya mapenzi na njia za kutumia kujikinga na mimba ya haraka na pia
umuulize hasa kuhusu kutumia dawa zenye progesterone na madhara yake
kwako. Vidonge hivi vinaathiri maziwa (kwa wingi na ubora) kwa kiwango
kidogo zaidi ukilinganisha na vidonge vyenye oestrogen.
Mwili wako umefanya kazi kubwa sana ya kuleta kiumbe duniani. Sio tu kwa
sababu ni utambulisho wako na kukufanya uitwe ‘mama’ na chochote
utachofanya kitakachokufurahisha, utashangaa jinsi ulivyo na sehemu
nyingi zinazoweza kukufanya upate raha.
Friday, August 24, 2018
Baada ya Muda Gani Unaruhusiwa Kufanya Mapenzi na Mkeo Baada ya Kujifungua?
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment