Katika harakati za kutafuta kazi nilibahatika kufika ofisi moja maeneo
ya Mwenge (Dar es salaam) kwangu ilikua faraja kubwa sababu kiukweli
nilikua nahangaika sana na hali ya ugumu wa maisha na sikutaka kabisa
kuwa tegemezi kwa mtu yoyote (wakiwemo wazazi) niliamini kunipa elimu ni
mtaji muhimu na tosha na lilikua jukumu langu kuandaa maisha yangu
mwenyewe na kujitegema
Nilipofika pale niliomba kuonana na boss ila nikaambiwa haiwezekani
labda ningekua na appointment, kutokana na uzoefu hii kauli nilikua
nimekutana nayo mara kadhaa hivyo ilikua hainisumbui sana, nikamwambia
yule receiptionist kuwa nilikua na appointment (kiukweli sikua nayo na
nakiri nilidanganya na nilikosea ila sikuwa na namna mbadala) akaniuliza
nimwambie we ni nani nikasema mwambie (tax consultant)
Waliongea mawili matatu then nikaruhusiwa kuingia nadiriki kusema shida
ni mwalimu mkubwa sana kwani sikuwa na woga wowote kuonana na yeyote na
kujinadi, baada ya mazungumzo na mahojiano ya kama dakika sita yule
manager (mwanamke) akaniambia alhamisi niende nikafanye interview na
kutokana na intro niliyoitoa hiyo siku (Jumanne).
Haikua kazi kwangu kupata hiyo kazi hata baada ya interview ya alhamisi,
tulikubaliana terms za kazi na mshahara then nikapewa mkataba.
Nilifurahi sana nikijua sasa mipango yangu itaenda vema (kwakweli
mshahara ulikua mzuri tu) hadi nikaanza kupangilia biashara ndogondogo
ili kuinua uchumi wangu.
Nilianza kazi wiki iliyofuata na wafanyakazi wenzangu walikua watu wema
sana kwangu hivyo nilifanya kazi kwa furaha na ufanisi sana mpaka hali
ilipokuja kubadilika.
MABADILIKO
Baada ya wiki moja mambo yalianza kubadilika pale ofisini, mara kwa mara
boss alikua na vikao visivyokua na mbele wala nyuma na mimi na akawa
mkali kwa wafanyakazi wenzangu especially wa kike na taratibu wakaanza
kuniogopa.
Siku moja aliniita ofisini (ilikua Ijumaa) na akaniambia nifunge mlango
nilishtuka sababu normally ukiingia ofisini lazima ufunge mlango cha
kushangaza akaniambia ni-u lock nikafanya alivyotaka,
Hakuna cha maana alichoniambia zaidi ya story za kifamilia tu oooh mara
mumewe (aliekuwa meneja kabla hajaumwa) anasumbuliwa na kisukari na
presha na anapata taabu sana mi nikawa msikilizaji tu na aliongea muda
mrefu hadi jua likazama na watu waliondoka ofisini alibaki mlinzi tu.
Aliongea mengi na mwisho akaniambia anataka nimsaidie (ngono) kitu
ambacho kilinishtua kidogo ukizingatia ni mtu mzima rika la mamaangu,
nilimbembeleza kuwa hapo si pahali salama ili tu aniache siku hiyo ili
nikajipange jinsi ya kuepukana nae na kuikabili ile hali.
Alinikomalia sana hadi kunivamia physically na alionekana wazi alikua
desperate for sex ila nilifanikiwa kumpanga na akanielewa baada ya hiyo
siku ofisi nzima wakahisi nilizini na yule boss hivyo kukawa na
minong'ono mingi na sikuwa na namna ya kuwaaminisha vinginevyo.
Tangu hapo ni wiki ya pili sasa huyu mama ananisumbua sana, ananiahidi
mambo mengi kama nitakubali kusex nae na ni dhahiri nikimtamkia kuwa
SITAKI nitapoteza kibarua kwani ye ndo meneja hapa na ndo anaajiri na
kusitisha ajira,
Leo hii (Jmosi) kanipigia simu na kuniambia kesho saa saba ana kikao na
mimi cha kikazi ila location naona hata aibu kuisema. Wakuu najua kuna
watu humu wakike na kiume ambao wamekutana na hali kama yangu,
Naipenda kazi na sina pa kushikilia kwa sasa lakini pia sitaki kuisaliti
imani yangu na msimamo kwa kupenda vitu vya dezo na kufanya uzinzi na
mtu wa rika la mama yangu, ni dhambi kubwa na pia ni kinyume cha maadili
ya jamii yetu lakini pia nikifikiria matokeo ya kuachishwa kazi (na
mipango niliyokwisha iweka kichwani kwangu) roho inaniuma sana nabaki
nikiwaza na kuwazua bila kujua haswaa nishike wapi.
Msimamo wangu ni kutokulala na huyu mama no matter the consequences ila
naomba mnipe chakula cha akili ili akinifukuza kazi basi niwe
nimeimarika kisaikolojia kwa ushauri wenu na nisitetereke sana
kisaikolojia.
Asanteni
Sunday, August 19, 2018
Boss Ananitaka Kingono, Nipo Njia Panda Naomba Ushauri
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment