Wakati
umemualika mwanamke sehemu unayoishi ama wakati umetoka deti katika
bar, unapaswa kujua ya kuwa kumsisimua mwanamke huanza kabla ya nyinyi
wawili kulala pamoja.
Unapaswa kumsisimua kuanzia nafasi ya kwanza ambayo utaipata kutoka
kwake. Kufanya hivyo kutamfanya akutake hata zaidi na kumfanya ajiandae
na mapema kabla hata kulala naye. Lakini ni mbinu gani inayoweza
kutumika kumsisimua mwanamke kabla hamjalala pamoja?
Zama nami...
Kutumia maneno
Maneno yanaweza kumsisimua mwanamke asilimia mia. Mwanzo wanawake
husisimuliwa na vitu wanavyosikia zaidi kuliko wanavyoona. Hii ndio
tofauti kuu kati ya jinsi ya kumsisimua mwanaume na mwanamke. Hauhitaji
kuonekana mchafu wakati ambapo unamsisimua mwanamke kwa kutumia maneno.
Mwanzo anaweza kusisimulika na jinsi ambavyo anakusisimua wewe. Unaweza
kumwambia maneno kama "Siwezi kungojea ile siku ambayo nitakuwa pekeangu
na wewe", "Nimeanza kuingiwa na mawazo nikifikiria hio nguo uliyovaa
inaficha nini" ama maneno mfanano na haya.
Lakini kando na kuwa maneno yanamsisimua mwanamke, kutategemea pia na vile ambavyo unamshika na miguso yako.
Kutumia miguso
Hapa ndipo utaleta utofauti wa yote. Miguso ni mbinu nzito na ya nguvu
kama unaazimia kumfanya akutamani, kabla hata nguo za yeyote kuvuliwa,
kabla ya nyinyi wawili kuanza kubusiana ama kufanya chochote. Baadhi ya
mifano ya kufuata ya kumsisimua mwanamke kwa miguso ili aweze kukutamani
kabla ya nyinyi wawili kulala pamoja ni kama ifuatayo: [Soma: Hatua za kumfanya mwanamke awe huru unapomgusa]
Kuzivuta nywele zake kiulaini: Usizivute nywele zake hadi ukazing'oa kichwani mwake. Lakini usiogope kuzishika baadhi ya nywele zake na kuzichezea kimvuto.
Miguso ya kukawia: Wakati ambapo unamgusa kikawaida - kwa mfano,
wakati mikono yako iko katika mabega yake, mgongo au mkono - usiogope
kuuzuia mkono wako ukawie sehemu hizo kwa dakika moja.
Karibu kumla dende: Hii ni siri kubwa ambayo inahakikisha gemu
yako kuwa ya juu. Usikimbilie kumbusu. Jiweke katika hali ambayo nyinyi
wawili mko "karibu" kubusiana. Hii itamfanya aingiwe na wazimu wa kutaka
kuibusu midomo yako haraka kuliko ulivyokuwa ukitarajia.
Kumkwaruza kiulaini: Unapomgusa, usiogope kuzipitisha kucha zako
kwa mgongo wake, nyuma ya shingo yake na sehemu mfanano na hizi. Hii
unaweza kuitumia wakati ambapo mshajenga uhusiano wa ndani kati yenu.
Mtizamo wa macho: Kumuangalia mwanamke kwa macho pekee kunaweza
kumfanya apandwe na mzuka. Mwangalie machoni, zaidi kuliko yeye. Kufanya
hivyo kunaashiria ujiaminifu. Ijapokuwa mbinu hii haitumii miguso,
inaweza kufanya kazi sawa na kama vile matumizi ya miguso kabla nyinyi
wawili kulala pamoja.
Ok hizi ni baadhi ya mbinu za kumfanya mwanamke asisimke kabla kulala na yeye. Unaweza hata pia kuamua kumpandisha nyege bila kutumia miguso yeyote.
Sambaza:
Tuesday, August 21, 2018
Jinsi Ya Kumsisimua Mwanamke Kabla Ya Kulala Naye
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment