Naamini mapenzi hayalazimishwi wala hayashikiwii Mtutu.
Pia naamini kwa dhati kabisa penzi linapokwisha ni bora watu watengane tu. Hakuna ndoa kama upendo haupo au maelewano hayapo.
Ndoa ni maelewano na makubaliano ya watu walio oana kimtazamo,kiuchumi,
kidini na mambo Kede Kede. Haya yanapokosekana hakuna ndoa na
usilazimishe upendo..
Kuna upuuzi fulani wa kumfumania mtu na kumlawiti mwanaume mwenzako au kumuua kabisa
Mimi naamini wanawake ni watu timamu na wenye maamuzi sahihi kabisa. Ukiona mke wako amekusaliti, achana naye.
Ukristo unaruhusu ndoa kuvunjika sababu ya uzinzi lakini pia hairuhusu
kisasi kwa namna yoyote ile wala hauruhusu kuua mtu sababu ya usaliti.
Mara nyingi wanawake hutoka na kutafuta wanaume wenyewe. Lakini hata
akitafutwa ana haki ya kukataa. Kuna wakati wanawake wengine huvua hata
pete za ndoa mavyuoni humu na hata maeneo mengine
Kulazimisha mapenzi ni ujinga wa kiwango chake. Mpe mwanamke mziki aupendao uone kama atatoka kama umeoa mke kweli.
Kulikuwa na mwanamke fulani anakwenda kusema kwa mume wake kila
akitongozwa. Siku kasema katongozwa na fulani na mume anamfahamu kaenda
speed kwa jamaa. Kufika kule ugomvi ukaanza. Jamaa mwenye mke kapigwa na
kupata ulemavu mpaka leo. Nani kasababisha haya?. Mke bila shaka.
Nimalizie kwa kusema huwezi kummiliki mtu. Mtu ana moyo wake na maamuzi
yake. Mtendee wema mkeo na kama yuko kamili hatokusaliti. Lakini kama
ulioa yule wa mwanaume mashine usiingie hatiani kuua au kulawiti
mwanaume mwenzako sababu ya maamuzi ya mtu aliye timamu kabisa.
Mabaya mawili hayaleti usahihi.
Thursday, August 23, 2018
Home
/
Unlabelled
/
Kumlawiti Mwanaume Mwenzako Sababu ya Kumfumania na Mkeo ni Ujinga wa Kiwango Chake
Kumlawiti Mwanaume Mwenzako Sababu ya Kumfumania na Mkeo ni Ujinga wa Kiwango Chake
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment