Kwangu kipindi ambacho kilinivutia sana ni kipindi cha kampeni za uchaguzi nchini Marekani.
Ni pale Obama akiwa katika kampeni kwenye moja ya majimbo kugombea duru
ya pili ya uraisi aliposimamisha hotuba yake na kutambua uwepo wa mkewe
Michelle.
Obama alisema, "Mke wangu amekuwa bega kwa bega na mimi tokea niko chuo,
kuna kipindi nilishindwa kulipa ada ila yeye ndiye aliyenilipia"
Obama akaenda mbali zaidi na kukiri mbele ya jamii ya kimataifa kwamba asingekuwepo hapo alipo kama sio mke wake Michelle.
Hivyo basi, nashauri kwamba mwanamke ambae mwanaume atakua nae huenda
akawa chachu ya mafanikio na baraka kwake au anaweza akamrudisha nyuma
kabisa katika mipango yake.
Sababu kuu 7 za kwanini iwe isiwe mwanaume lazima upate mwanamke alie sahihi.
1. Kila mwanamke anao uwezo wa kukuridhisha kimapenzi ila mwanamke
sahihi na bora pekee ndiue anaeweza kuku-challenge kiakili na kuwa
'intellectually inspired'.
2. Mwanamke yeyote anaweza kukuteka kihisia, ila yule sahihi pekee ndiye
mwenye uwezo wa kukuteka kiroho na ukamtumikia Mungu wako.
3. Mwanamke yeyote anaweza akakushawishi muandike mpango wa harusi
(wedding plan), ila mwanamke sahihi peke yake ndie mwenye uwezo wa
kukuandikia na kukushauri mpango wa biashara (business plan)
4. Kila mwanamke anaweza akakubusu tena 'French kiss' ila mwanamke bora
pekee ndio mwenye uwezo wa kukutamkia maneno yaliyojaa busara na hekima.
5. Kila mwanamke anaweza akakupenda sana tu tena kama una pesa, ila
mwanamke aliye bora pekee ndiye anaeweza kusimama na wewe hata kukuinua
pale utakapokuwa huna kitu.
6. Mwanamke yeyote anao uwezo wa kukushibisha kwa kukupikia chakula
kitamu, ila mwanamke bora pekee ndio mwenye uwezo wa kukulisha chakula
cha ubongo.
7. Kila mwanamke anao uwezo wa kukushawishi chumbani ila mwanamke bora
pekee ndio mwenye uwezo wa kukushawishi umrudie Mungu wako.
Mwisho ngoja nihitimishe kwa kusema hivi ukisoma vitabu vya kihistoria
kuhusu Winstom Churchhill mpaka Abraham Lincoln, na kutoka kwa Nelson
Mandela mpaka kwa Martin Luther King Jr lao moja kwamba “No matter how
strong a Man is, he is only as strong as the Woman he marries” Kwa
tafsiri yangu ya kuunga unga isiyo sahihi sana Wanamaanisha "haijalishi
ni kwa kiasi gani mwanaume una nguvu, nguvu zako zina athiriwa kwa kiasi
kikubwa na mwanamke utakaemuoa"
Tuesday, August 21, 2018
Sababu kuu 7 za Kwanini Kila Mwanaume Anahitaji Mwanamke Sahihi
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment