Umepewa nambari ya simu na mwanaume/mwanamke unayemzimia na hujui aina
gani au ngapi za meseji unazotaka kumtumia? Cheza kwa ujanja ukitumia
sheria hizi ambazo ni lazima yeyote anafaa kutumia ikija maswala ya
kumtext yeyote aliyemzimia.
1. Mtext unayemzimia kwa maswali rahisi
Kama unamtaka yule uliyemzimia ajibu texts zako, lazima utoe sababu
muhimu kwake kujibu texts zako. Unaweza kuanza kumtext kwa kumuuliza
anafanya nini muda huo ama unaweza kumtext na kitu ambacho mlikuwa
mkifanya pamoja wakati uliopita. Mfano unaweza kumtext 'Ile story ya
kuenda kumtembelea binamu yako ilifikia wapi?' [Soma: Maswali mazuri ya kumuuliza mwanamke]
2. Usingojee ajibu meseji ukiwa hapo
Iwapo amejibu text yako kwa haraka ni vyema. Lakini kama atachukua muda
mwingi, usijisumbue kamwe kukaa karibu na simu. Tafuta kazi nyingine ile
ujikeep buzy usijishughulishe na kufikiria meseji uliyomtumia.
3. Usimtext unayemzimia meseji nyingi wakati mmoja
Usijaribu kutuma zaidi ya meseji moja kabla hajakujibu. Hii itaondoa ile
hisia ya kuonekana kama mtu mwenye tamaa ama kuonekana kama una ajenda
chafu. Hii itajitokeza iwapo kama huyo unayemzimia hujakuwa na mazoea
naye.
4. Mazungumzo yenu yaendelee...hadi pale kikomo
Iwapo maongezi yenu yanaendelea vizuri basi ni vyema. Hakikisha ya kuwa
usipitishe maongezi yenu mpaka yaingie kitengo cha kuboesha. Ukiona
unayemzimia anachukua muda mrefu kujibu texts zako ama kujibu kwa neno
moja moja, basi fahamu ya kuwa maongezi yenu yamefika kituo na unafaa
kusmamisha texts zenu hadi siku nyingine.
5. Endeleza maongezi binafsi
Kutumia mtu meseji ni rahisi sana kwa kuwa inatoa tenshen na wasiwasi.
Pia meseji husaidia mtu kujieleza zaidi. Lakini unafaa kufahamu ya kuwa
meseji pekee haziwezi kumshawishi mtu kwa kiwango kikubwa hivyo unafaa
ufuatilie wewe binafsi ukutane na unayemzimia ili uendeleze maongezi
yenu. [Soma: Jinsi ya kuapproach mwanamke usiyekuwa na mazoea naye]
6. Tafuta ishara kubwa kama unayemzimia hajakupenda
Je wewe ni yule ambaye wakati wote unaanza kumtext huyo uliyemzimia? Je
unayemzimia ni yule ambaye anakutumia text wakati wa shida na hawezi
kukutext wakati mwingine? Hii ni dalili ya kuonyesha ya kuwa yule
unayemtext kwa kawaida anafanya hivyo ili kuondoa uchoshi kwake ama
anafanya hivyo kukuonyesha tu heshima kwako.
Ukiona mtu anamiliki aina hii ya tabia basi ni ishara ya kukuambia ujipatie shughli na utafute kwingine. [Soma: Utajuaje kama mwanamke anakupenda]
Monday, August 20, 2018
Sheria Za Kufuata Unapomtumia Meseji Uliyemzimia
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment