Utafiti
wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) umebaini kuwa asilimia 33
ya wanaume 672 mkoani Dar es salaam wamebainika kuwa na upungufu wa
nguvu za kiume.
Hayo
yamezungumzwa na Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo Dk. Pedro Pallangyo
ambaye ameeleza kuwa idadi kubwa ya wagonjwa hao wanasumbuliwa na
tatizo kubwa la shinikizo la damu na kisukari.
Utafiti huo uliofanywa na JKCI, umebainsisha kuwa katika wanaume watatu mmoja aligundulika kukosa nguvu za kiume.
”Hali
hii inaashiria kuwa magonjwa ya kisukari na shinikizo la damu yamekuwa
yakiongezeka mara kwa mara jambo ambalo linasababisha athari ya nguvu za
kiume kuwa kubwa ,” amesema Dk. Pallnagyo.
Aidha
amesema changamoto hiyo inaweza kutatuliwa iwapo jamii itakuwa na
utaratibu wa kufanya uchunguzi wa afya zao mara kwa mara ili kugundua
tatizo mapema na kupata matibabu.
Pia
alichukua nafasi kutoa ushauri kwa wanaume kupunguza sana matumizi ya
chumvi nyingi mwilini na kupunguza kula vyakula vyenye mafuta mengi
kwani hivyo huchangia kwa kiasi kikubwa sana magonjwa ya shinikizo la
damu na kisukari na kupelekea nguvu za kiume kushindwa kufanya kazi yake
kama mabavyo inatakiwa.
No comments:
Post a Comment