WENYE MSIMAMO Wanawake
daraja la kwanza wanaopendwa zaidi na wanaume ni wale wenye msimamo,
uelewa mkubwa wa mambo na maamuzi sahihi, wako makini kwenye matendo yao
na siku zote hufanya vitu kwa ajili ya kupata mafanikio.
WAPENDA USAWA Aina
ya pili inayohitajika katika katika ulimwengu wa kimapenzi ni wanawake
wanaoheshimu usawa wa jinsia, walio tayari kubeba majukumu ya kifamilia
kwa ulinganifu sawa na wanaume, wenye uwezo wa kuongoza jamii kwa
asilimia 50 kwa 50.
WANAOJUA MAPENZI Wanawake
wajuzi wa mambo ya faragha wanapendwa sana. Sifa yao kubwa ni uwezo wa
kutosheleza katika tendo la ndoa. Tafiti zinaonyesha kuwa wanaume
hupenda sana wanawake watundu katika mchezo wa sita kwa sita. Mara
nyingi wanatajwa kuwa na uwezo wa kuteka akili za wanaume bila kujali
sifa zao za nje au za ndani.
MARAFIKI Wanawake
wenye sifa sawa na rafiki ni aina ya nne inayowavutia wanaume. Wao
hutegemea zaidi nguvu ya kushawishi inayotokana na namna wanavyojali na
kujitolea kuhakikisha wanakuwa marafiki wa kweli kwenye shida na raha
kwa wapenzi wao. Si wakorofi, waungwana na wapenda amani. WA WAZI Aina
nyingine ya wanawake inayowavutia wanaume ni wenye msimamo na uwazi. Si
wepesi wa kuburuzwa katika maamuzi ya msingi kwa kisingizio cha wao ni
wanawake. Utafiti unaonesha wanawake wa aina hii wamekuwa muhimu hasa
kwa wanaume wenye tabia za ubabe na udhaifu katika uelewa wa mambo.
WANAOJITEGEMEA Wanawake
wanaojitegemea wana soko kubwa kwa wanaume tofauti na akina naomba
vocha kila siku. Uchunguzi unaonyesha kuwa wanaume wa leo hawapendi
wanawake tegemezi, wasiokuwa na kazi na wanaoendekeza starehe za upande
mmoja. WASIO NA PRESHA Nikisema
wanawake wasiokuwa na presha namaanisha wasiolazimisha vitu vitokee
haraka haraka. Wao siku zote huacha mambo yatokee yenyewe na kazi yao
kuwa ni kutenda sehemu ya majukumu yao kama wapenzi.
MARIDADI Kundi
lingine la wanawake wanaopendwa na wanaume ni wanaozingatia usafi na
kujiremba. Wanaokwenda na wakati katika mavazi na mvuto wa nje. Lakini
pia ni welewa wa mazingira, si wasamba. Wanapendeza kwa muonekano. WANAORIDHIKA Wanawake
ambao hulidhika na hali walizonazo ni kivutio kikubwa kwa wanaume, hili
ni kundi linalohitajika sana katika ulimwengu wa mapenzi kwa upande wa
wanaume ambao maisha ya sasa yamekuwa yakiwageuza kutoka juu kwenda
chini au chini juu. Kukubali hali zote bila kubadili tabia ni sifa njema
ya mwanamke. WA MMOJA Wanawake
wanaochagua mara moja na kutosheka na kuwa tayari kukwepa kila aina ya
vishawishi toka kwa wanaume ambao kimtazamo wana vitu vya ziada zaidi ya
waliowachagua mwanzo wanahitajika sana. “Niliye naye ananitosheleza kwa
kila kitu sitaki mtu mwingine.” Kundi la wanawake wa aina hii ni adimu
na muhimu sana.
No comments:
Post a Comment