Kampuni ya teknolojia ya Google imewafuta kazi watu 48 wakiwemo maafisa
13 wakuu kutokana na tuhuma za unyanyasaji wa kingono tangu 2016.
Kwa mujibu wa BBC, Katika barua kwa wafanyakazi wake, mkurugenzi mmkuu
mtendaji Sundar Pichai amesema kampuni hiyo kubwa ya teknolojia
inachukua ‘msimamo mkali’ dhidi ya tabia zisizo sawa.
Barua hiyo inafuata ripoti ya New York Times kwamba muasisi wa mfumo wa
Android Andy Rubin alipokea $90m kama kititia cha kuondoka licha ya
kukabiliwa na tuhuma za utovu wa nidhamu.
Msemaji wa Bwana Rubin alikana tuhuma hizo, gazeti hilo limesema.
Sam Singer amesema Bwana Rubin aliamua kuondoka Google mnamo 2014 kuanzisha kampuni yake ya teknolojia kwa jina Playground.
‘Aliagwa kama shujaa’ wakati alipoondoka, gazeti hilo linasema.
Barua ya Pichai inasema ripoti ya New York Times ni “ngumu kuisoma” na
kwamba Google “inachukulia kwa uzito” suala la kutoa “nafasi salama ya
kazi na inayotoa fursa kwa usawa”.
Muasisi wa mfumo wa Android Andy Rubin aliondoka Google mnamo 2014
“Tunataka tuwahakikishie kwamba tunatathmini malalamiko yote kuhusu
unyanyasaji wa kingono au utovu wowote wa nidhamu, tunachunguza na
tunachukua hatua,” aliendelea.
Hakuna mfanyakazi aliyetimuliwa katika miaka miwili iliyopita aliyepokea kitita cha kuondoka Pichai ameongeza.
Kwa mujibu wa ripoti ya New York Times, wakurugenzi wawili wa Google,
wameeleza kuwa aliyekuwa mkurugenzi mkuu mtendaji Larry Page aliomuamba
bwana Rubin kujiuzulu baada ya kampuni hiyo kuthibitisha malalamiko ya
mfanyakazi mwanamke kuhusu tnedo la ndoa lililofanyika katika chumba cha
hoteli moja mnamo 2013.
Rubin alisema hakufanya utovu wowote wa nidhamu na aliondoka Google kwa hiari yake.
Tuhuma hizi zinaongezea malalamiko kuhusu kukanwa kwa utamaduni ulioko
unaoshinikiza unyanyasaji wa kingono katika kampuni hiyo iliyo na idadi
kubwa ya wanaume.
Hisa za Alphabet, inayoimiliki kampuni ya Google, zimeshuka kwa zaidi ya
3% New York baada ya kutangaza mapato ya $33.7bn kwa miezi mitatu hadi
Septemba – kiwango kilicho chini kidogo na kilichotarajiwa na
wacahambuzi.
Hatahivyo faida jumla ilikwea kutoka $2.5bn hadi $9.2bn – kiwango cha juu zaidi ya ilivyotarajiwa.
Saturday, October 27, 2018
Google yawatimua Kazi Watu 48 Wakiwemo Maafisa wake wakuu Kwa Tuhuma za Ngono
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment