Artikel Terbaru

Responsive Ads Here

Thursday, October 25, 2018

Huyu Binti Nimempata Mwezi wa Tatu Sasa Hajaniomba Hela Nimueleweje


Kuna binti mmoja umri miaka 23 sasa ni miezi mitatu tangu nimtokee cha kushangaza hajaniomba hata mia tano ya vocha na ni mwanafunzi sasa nimueleweje maana kwangu imekuwa kama muujiza, hao wanaofanya kazi tu tayari ni makamanda wa kikosi cha mizinga siku mbili tu ukiwa nae tayari atakuangushia jumba bovu

Juzi nimetoka out nae wakati namuaga nakampa eflu hamsini ila cha ajabu aliniridishia akaniambia she is fine ...yaani mpaka namuogopa sasa

Binti ni mrembo sana na inaonekana anatoka familia ya kawaida sana ..Je Niwekeze hapa Kimoja naona dalili ya Mke mwema..Au bado naliliwa Timing?

No comments:

Post a Comment