Ikija katika maswala ya kuwavutia wanawake, kile kitu ambacho utamtamkia kitakusaidia pakubwa katika azma yako ya kumuwini.
Hakuna ujanja wowote ambayo unatumika bali ni maneno yako. Wanawake ni
viumbe ambao ni wasikilivu ilhali wanaume ni viumbe waangalifu, hivyo
matumizi yako ya maneno ni silaha nzito ambayo umebarikiwa nayo.
Ok. Ikija katika usikilizi, kila mwanamke huwa tofauti. So itabidi
umsome mwanamke kwanza na uyafahamu mambo gani anapenda ili ikija wakati
wa kumtamkia maneno itakuwa rahisi kwako kumteka kihisia. Tumeandaa
orodha ya maneno ambayo ukiyatumia yapasavyo yatakusaidia kumzuzua
mwanamke yoyote awe rafiki yako ama mpenzi wako. Zama nasi.
#1 Yuko smarti. Hapa hauwezi kukosea wakati utakapomwambia kuwa
anapendeza. Unachohitajika ni kumtamkia maneno kama haya wakati ufaao.
Unaweza kumweleza sehemu ambayo unaona yuko smarti na utakuwa
unamfurahisha wakati wote.
#2 Unapenda jazba na msukumo wake. Kama umeona kuwa mwanamke aina hii
ana ari na msukumo wa kufanikisha jambo flani basi unapaswa kumpongeza.
Kama hana msukumo wowote katika maisha halafu umsifie atashangaa
unamsifia na nini. So hakikisha kuwa unampa sifa aina hii kulingana na
msukumo wake wa kutimiza jambo fulani katika maisha yake.
#3 Unapenda vyenye anavyoishi. Hapa unamsifia maisha yake yote. Hii ina
maana kubwa katika kila kitu cha maisha yake. Wakati unapomtamkia maneno
kama haya hakikisha kuwa unakuwa serious na kile ambacho unatamka.
#4 Kuwa yeye ni muhimu kwako. Kama unajaribu kumuonyesha mwanamke kuwa
unamweka kipao mbele katika maisha yako unapaswa umwambie kuwa yeye ni
muhimu katika maisha yako. Haya ni matamshi mazito ambayo utamfurahisha
na kutamani kuwa na wewe milele.
#5 Yeye ni tofauti na wengine. Kila mwanamke anatamani kuwa spesho.
Wanatamani kuwa tofauti na wanawake wengine wale wote. So msifie
mwanamke na umwambie kuwa yeye ni tofauti, hakuna mwanamke mwengine
ambaye anaweza kufikia kiwango chake. Utafaulu kumuwini.
#6 Unajali maslahi yake. Wanaume wengi mara nyingi huwa wanashindwa
kutamka maneno haya mbele ya mwanamke japo kuwa ni matamshi rahisi ya
kusema. Hapa si lazima uingie ndani ueleze sababu zako zote. Kumtamkia
maneno kama haya yanatosha kwa mwanamke.
#7 Ni mrembo zaidi ya maumbile. Hapa unatuma ujumbe wakumwambia kuwa
yeye kando ya kuwa ni mrembo kimwili, pia ni mrembo ndani yake. Mweleze
kinjia ambayo hakutaleta kana kwamba ni mrembo kimaumbile pekee.
#8 Anakusisimua bila hata kujaribu chochote. Hii ni silaha nzito
unapaswa kuitumia kwa kuwa wanawake wengi hupenda kuskia matamshi kama
haya. Wanawake wana hisia ndani zao so ukimtamkia maneno kama haya
watahisi kujishasha/sifu hivyo wataskia vizuri ndani yao.
#9 Kama anataka kuongea uko tayari kumsikiliza. Hii inaweza kuonekana
kama ni mambo ya friend zone lakini ukweli ni kuwa wanawake hupenda
kusikilizwa na wapenzi wao. Hii inamaana kuwa uko tayari kutenga nafasi
yako spesheli ili uongee naye. Atajihisi tofauti.
#10 Utakuwa karibu naye kwa shida na raha. Mwanamke anataka utumishi
kutoka kwako. Kama una upendo ndani yako kwake, basi atahisi usalama,
kukamilika na kupendwa. Hivyo baada ya kusoma hii post spesheli
tulioiandika hapa Nesi Mapenzi, unapaswa kumtamkia maneno haya mpenzi
wako.
#11 Unataka kusapoti ndoto zake. Wanawake huwa na ndoto zao katika
maisha. Hivyo ukionyesha usaidizi wako kwake kutamfanya akuthamini na
kukupenda zaidi. Usisahau swala hili muhimu katika mapenzi.
#12 Unamshukuru kwa kila kitu. Kuwa katika relationship lazima pia uwe
unaeleza hisia zako kwa mpenzi wako. Na njia moja ya kufanya hivi ni kwa
kumshukuru mpenzi wako kwa kila jambo ambalo ameweza kukufanyia katika
maisha yako.
#13 Unataka ushauri wake. Wanawake pia hupenda maoni yao yasikilizwe
kuhusiana na jambo fulani. So usichelewe kumuuliza ushauri mpenzi wako
hata kama ni jambo dogo. Hilo hilo dogo litamfanya kuona unathamini
uwepo wake.
#14 Mwambie kuwa una plan nzuri ya nyinyi wawili. Wanawake wangependa
kuona kuwa wapenzi wao wanapanga mambo ya usoni katika maisha wakiwa
wamehusishwa. Hili ni jambo muhimu ambalo wanawake wangependa kusikia
wapenzi wao wakiwatamkia.
Ok. Upo!? Haya ndio baadhi ya mambo ambayo wanawake wanatamani kuskia
kutoka kwa wapenzi wao hivyo unapaswa kuchangamka sahizi na kutafuta
maneno ambayo yanawiana na mpenzi wako sahizi.
Friday, October 19, 2018
Maneno 14 Ambayo Mwanamke Anatamani Umwambi
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment