Ikija katika maswala ya kuwavutia wanawake, kile kitu ambacho utamtamkia kitakusaidia pakubwa katika azma yako ya kumuwini.
Hakuna ujanja wowote ambayo unatumika bali ni maneno yako. Wanawake ni
viumbe ambao ni wasikilivu ilhali wanaume ni viumbe waangalifu, hivyo
matumizi yako ya maneno ni silaha nzito ambayo umebarikiwa nayo.
Ok. Ikija katika usikilizi, kila mwanamke huwa tofauti. So itabidi
umsome mwanamke kwanza na uyafahamu mambo gani anapenda ili ikija wakati
wa kumtamkia maneno itakuwa rahisi kwako kumteka kihisia. Tumeandaa
orodha ya maneno ambayo ukiyatumia yapasavyo yatakusaidia kumzuzua
mwanamke yoyote awe rafiki yako ama mpenzi wako. Zama nasi.
#1 Yuko smarti. Hapa hauwezi kukosea wakati utakapomwambia kuwa
anapendeza. Unachohitajika ni kumtamkia maneno kama haya wakati ufaao.
Unaweza kumweleza sehemu ambayo unaona yuko smarti na utakuwa
unamfurahisha wakati wote.
#2 Unapenda jazba na msukumo wake. Kama umeona kuwa mwanamke aina
hii ana ari na msukumo wa kufanikisha jambo flani basi unapaswa
kumpongeza. Kama hana msukumo wowote katika maisha halafu umsifie
atashangaa unamsifia na nini. So hakikisha kuwa unampa sifa aina hii
kulingana na msukumo wake wa kutimiza jambo fulani katika maisha yake.
#3 Unapenda vyenye anavyoishi. Hapa unamsifia maisha yake yote.
Hii ina maana kubwa katika kila kitu cha maisha yake. Wakati
unapomtamkia maneno kama haya hakikisha kuwa unakuwa serious na kile
ambacho unatamka.
#4 Kuwa yeye ni muhimu kwako. Kama unajaribu kumuonyesha mwanamke
kuwa unamweka kipao mbele katika maisha yako unapaswa umwambie kuwa
yeye ni muhimu katika maisha yako. Haya ni matamshi mazito ambayo
utamfurahisha na kutamani kuwa na wewe milele.
#5 Yeye ni tofauti na wengine. Kila mwanamke anatamani kuwa
spesho. Wanatamani kuwa tofauti na wanawake wengine wale wote. So msifie
mwanamke na umwambie kuwa yeye ni tofauti, hakuna mwanamke mwengine
ambaye anaweza kufikia kiwango chake. Utafaulu kumuwini.
#6 Unajali maslahi yake. Wanaume wengi mara nyingi huwa
wanashindwa kutamka maneno haya mbele ya mwanamke japo kuwa ni matamshi
rahisi ya kusema. Hapa si lazima uingie ndani ueleze sababu zako zote.
Kumtamkia maneno kama haya yanatosha kwa mwanamke.
#7 Ni mrembo zaidi ya maumbile. Hapa unatuma ujumbe wakumwambia
kuwa yeye kando ya kuwa ni mrembo kimwili, pia ni mrembo ndani yake.
Mweleze kinjia ambayo hakutaleta kana kwamba ni mrembo kimaumbile pekee.
#8 Anakusisimua bila hata kujaribu chochote. Hii ni silaha nzito
unapaswa kuitumia kwa kuwa wanawake wengi hupenda kuskia matamshi kama
haya. Wanawake wana hisia ndani zao so ukimtamkia maneno kama haya
watahisi kujishasha/sifu hivyo wataskia vizuri ndani yao.
#9 Kama anataka kuongea uko tayari kumsikiliza. Hii inaweza
kuonekana kama ni mambo ya friend zone lakini ukweli ni kuwa wanawake
hupenda kusikilizwa na wapenzi wao. Hii inamaana kuwa uko tayari kutenga
nafasi yako spesheli ili uongee naye. Atajihisi tofauti.
#10 Utakuwa karibu naye kwa shida na raha. Mwanamke anataka
utumishi kutoka kwako. Kama una upendo ndani yako kwake, basi atahisi
usalama, kukamilika na kupendwa. Hivyo baada ya kusoma hii post spesheli
tulioiandika hapa Nesi Mapenzi, unapaswa kumtamkia maneno haya mpenzi
wako.
#11 Unataka kusapoti ndoto zake. Wanawake huwa na ndoto zao
katika maisha. Hivyo ukionyesha usaidizi wako kwake kutamfanya
akuthamini na kukupenda zaidi. Usisahau swala hili muhimu katika
mapenzi.
#12 Unamshukuru kwa kila kitu. Kuwa katika relationship lazima
pia uwe unaeleza hisia zako kwa mpenzi wako. Na njia moja ya kufanya
hivi ni kwa kumshukuru mpenzi wako kwa kila jambo ambalo ameweza
kukufanyia katika maisha yako.
#13 Unataka ushauri wake. Wanawake pia hupenda maoni yao
yasikilizwe kuhusiana na jambo fulani. So usichelewe kumuuliza ushauri
mpenzi wako hata kama ni jambo dogo. Hilo hilo dogo litamfanya kuona
unathamini uwepo wake.
#14 Mwambie kuwa una plan nzuri ya nyinyi wawili. Wanawake
wangependa kuona kuwa wapenzi wao wanapanga mambo ya usoni katika maisha
wakiwa wamehusishwa. Hili ni jambo muhimu ambalo wanawake wangependa
kusikia wapenzi wao wakiwatamkia.
Ok. Upo!? Haya ndio baadhi ya mambo ambayo wanawake wanatamani kuskia
kutoka kwa wapenzi wao hivyo unapaswa kuchangamka sahizi na kutafuta
maneno ambayo yanawiana na mpenzi wako sahizi.
Sunday, October 21, 2018
Maneno 14 Ambayo Mwanamke Anatamani Umwambie
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment