Artikel Terbaru

Responsive Ads Here

Monday, October 29, 2018

Mkali Wenu Akiri Kumtosa Ebitoke

Mchekeshaji maarufu kwenye mitandao ya kijamii Jackson Miraji maarufu kama Mkali Wenu ameibuka na kukiri kuwa amegoma kufanya kazi na msanii mwenzake wa vichekesho Anna Exavery maarufu kama Ebitoke pamoja na kumuomba sana.

Mkali wenu na Ebitoke waliwahi kufanya kazi pamoja siku za nyuma wakati wote Walipokuwa chini ya kundi la Timamu sikun za nyuma kabla ya Mkali wenu kuondoka wa kwanza na kufuatiwa na Ebitoke.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Mkali Wenu alisema baada ya Ebitoke kutoka katika Kundi la Timamu alimtafuta ili waungane wafanye kazi pamoja kama zamani lakini hakumkubalia kwa sababu bado anamfikiria asije akawa ana lake jambo na sio kwa nia njema ya kufanya naye kazi.

Ebitoke amenibembeleza sana tushirikiane baada ya yeye kutoka Timamu kwa madai ya kunyonywa na meneja na maslahi madogo ila sina mpango naye na wala sikuwahi kuwaza kama nitarudi kufanya naye kazi japo ombi lake bado nalifikiria na kupata maoni ya watu wangu wa karibu”.

No comments:

Post a Comment