Kuna dada mmoja nje ya nchi ambaye anataka kuja hadi hapa Sikonge ili
nimtungishe Mimba na hatimaye azae mtoto. Huyu mdada ni mtu ambaye
ninafahamiana naye kwa miaka mingi kidogo tangu nikiishi nje ya nchi
ambapo siku hizo, hakuwa au nilikuwa sijajua kama ni SHOGA.
Anasema yupo tayari kuwekeana kabisa mkataba na mie kwamba gharama zote
za mimba na kulea mtoto hatanidai na mtoto ataandikishwa kwa jina lolote
nitakalokubali mie na hata akitaka atanilipa. Sijui kaona kitu gani cha
ajabu kwa Mnyamwezi mie ingawa kiukweli hadi leo hii sijawahi hata
kumbusu, acha kutembea naye.
Kuhusu Mimba anasema inaweza kuwa kwa njia ya kawaida kwa kufanya
mapenzi au kwenda hospital na huko wakafanya kupandikiza kama
wanavyofanya kwa wale wanaotoa mbegu za Kiume na kuwapa akina mama ambao
hata hawawajui.
Shida kubwa iliyopo ni kuona kuwa Mtoto wangu anaweza kukulia kwenye
familia au nyumba ambayo Mama anaishi na GIRLFRIEND wake na kwa maana
nyingine ni kwamba, hawa ni Wasagaji. Mbaya zaidi kakiwa ka kike, si
ndiyo itakuwa shida kwa mtoto huyo? Itabidi ajifunze kuwa Mliberali
mapema sana au aungane nao.
Hebu nyie wakali na wazoefu wa haya mambo mniambie, kwa hili NIKUBALI au NIKATAE?
ANGALIZO: Hii ni habari ya kweli, utani pembeni Bandugu.
Thursday, October 4, 2018
MWANAMKE Msagaji Ameniomba Nimpe Ujauzito ili Azae Mtoto
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment