Imekuwa
miezi kadhaa tangu uachane na ex wako. Kwa sababu zisizoweza kuepukika
uliamua kukata uhusiano wako na mpenzi wako ili utafute maisha yako.
Lakini
kuna tatizo ambalo linajitokeza mara kwa mara. Kila ukikaa ama
kupumzika unamkumbuka ex wako. Na si kwa sababu unamtamani, la. Ex wako
umeachana naye na labda sahizi uko na mpenzi mwingine. Tatizo ni kuwa
huelewi ni kwa nini unaendelea kumkumbuka ex wako.
Well, sababu tunazo. Kuna mambo ambayo yanakufanya umkumbuke ex wako bila kukusudia. Na ni kama yafuatayo.
#1 Mko na marafiki ambao mnagawana.
Nyote wawili mko katika group moja. Mara nyingi kwa kawaida huwa
wapenzi wawili wanakuwa na marafiki wanaogawa. Rafiki yako anaweza kuwa
rafiki ya mpenzi wako hivyo kuna kuwa na mshikamano flani. Kama hali
kama hii imetokea kwako, kwa mfano katika mtandao rafiki yako anaweza
kurusha picha akiwa na ex wako hivyo unaweza kukumbuka hisia na upendo
ambao ex wako alikuwa akikuonyesha.
#2 Nilikuwa nikiagiza chakula changu hapa.
Je unakumbuka wakati ex wako ulikuwa ukienda nae katika hoteli flani
kila wakati kula chakula flani? Wazikumbuka zile hisia nzuri ambazo
ulikuwa ukizipitia huo wakati?
Hio
huwa ni kawaida. Kukumbuka kitu ambacho ex wako alikuwa akikufanyia
haimaanishi kuwa bado unamtamani. Inakuja tu kwa kuwa unakumbuka
ukumbusho ambao ulikuwa unapenda haswa wakati mlipokuwa mnakula pamoja.
#3 Nilikuwa hapa mwaka jana.
Nikiwa na ex wangu. Na leo umekuja katika sehemu hio hio na kumbukumbu
za wewe na ex wako zinajitokeza. Ni kawaida kuwa na kumbukumbu haswa
iwapo wewe na ex wako mlikuwa mnapenda kutembelea hio sehemu mara kwa
mara.
#4 Unamwona ex wako kila mahali.
Ni vigumu kumuona mtu ambaye umekuwa ukimjua halafu usiweze kuwafikiria
katika hali moja au nyingine. Kama umeenda katika mkahawa ukakutana na
ex wako, ama anafanya kazi katika shirikia flani na ni njia unayoipitia
kila siku basi ujue huwezi kumuondoa kwa akili yako.
Kumkumbuka
ex wako na kukumbuka mambo matamu na mazuri ambayo mmekuwa mkifurahi
ukiwa na ex wako ni vitu viwili tofauti. Kama ni kumbukumbu ambayo
imekuja tu kwa ghafla basi isiwe jambo kubwa la kutatiza. Itakuwa ni
akili yako tu ndio ilijaribu kukukumbusha yale mambo mazuri ambayo
ulipitia ukiwa na ex wako.
#5 Kizazi cha mitandao ya kijamii.
Mitandao ya kijamii ina manufaa na maafa. Kwanza ni kuwa unajiunga na
karibu kila mtu ambaye unajuana naye. So wakati ex wako anapost kitu
flani kwa mtandao, fikra zako zinakuja kutaka kujua ni kwa nini ex wako
amepost kitu kama hicho online.
Hii
ni kama tu vile marafiki zako katika mtandao wangependa kujua
umemaanisha nini baada ya kupost status flani. So fikra zao ni kama tu
zile fikra za marafiki zako katika mitandao ya kijamii, ikijumlisha ex
wako.
#6 Nguvu za hisia.
Miili yetu imeumbwa kiajabu. Unaweza kunusa ama kuona kitu halafu
ukakumbuka jambo flani. Hivyo hivyo unaweza ukakumbana na harufu ya
marashi flani halafu ghafla ukaanza kumkumbuka ex wako vile alivyokuwa
akipenda marashi hayo.
So
usichukulie uzito kwa kuwa hatuwezi kukontrol mawazo yetu, kwa sababu
akili yako itakuwa inajaribu kukukumbusha mambo ya zamani.
#7 Vitu ambavyo unamiliki.
Ukiachana na mpenzi wako haimaanishi kuwa kila kitu ambacho amekupatia
unafaa kumrudishia, la. Kuna wakati unawezakuwa na nguo ambazo
umenunuliwa, simu ama PS4. Hivi huwezi kuvitupa.
So
sahizi umeachana naye halafu ukakumbuka unashikilia kitu ambacho
umepewa na ex wako. Hii haimaanishi kuwa kumiliki vitu hivyo
kunamaanisha hutaki kumsahau ex wako.
#8 Mazungumzo ya miguso ya moyo.
Unaweza kuwa na marafiki zako halafu uanze kuwapa ushauri nasaha.
Halafu katika mazungumzo yako inakuja kwamba unawashauri kulingana na
experience umepitia ulipokuwa na ex wako. Kama itakuwa ngumu kuongea
kuhusu experience zako na ex wako basi inamaanisha kuwa una chembechembe
za hisia na ex wako. Lakini kama utaongea bila wasiwasi bila kuzua
hisia basi utakuwa uko sawa.
Kumbuka
kuwa kumkumbuka ex wako hakumaanishi kuwa unamtamani ama uko la
feelings na yeye. Kukumbuka zama za kale na kutamani zama za kale zirudi
ni mambo mawili tofauti. Kumbuka haya wakati fikra za ex wako zitakuja
tena.
No comments:
Post a Comment