Mapenzi ni matamu ukipata mpenzi mnaependana. Mahusiano mengi huvunjika
na chanzo kikuu huwa ni ‘uplayer’ kama ninavyopenda kuuita namba sita
mgongoni. Lakini wanaume wengi hujiuliza kwa nini mwanamke wangu
hatosheki na mimi. Tatizo litakuwa ni wewe mwanaume ndie unayechangia
ama pia labda ni mkewako ambaye ana shida. So leo hapa Nesi Mapenzi
tumekuja na majibu kamili uzijue kwa nini wanawake wengi huplay wanaume
zao.
#1 Tamaa. Tamaa huvunja mahusiano mengi. Si kila mwanamke
anapenda alivyo ilhali wengine wanaweza kuwa wanapenda pesa. Hivyo basi
kama wewe ni mwanaume na mfuko wako hauna kitu basi ujue si kila
mwanamke anaweza kuishi na wewe. Hivyo basi usitarajie uwe hauna kitu
ukadhani kila mwanamke anaweza kuvumilia na hali ulionayo. Mwanamke
hutafuta mwanaume atakayetimiza mahitaji yake na wewe uwe tu kama msaada
wake.
#2 Mapenzi. Je wewe uko bora kitandani. Swala hili mara nyingi
husumbua sana. Kila mwanamke ana kiwango chake cha kufika kileleni.
Mwanaume kama huwezi kumridhisha mkeo kitandani basi jua kuwa kunaweza
kutokea matatizo. Wanawake wengine hutafuta wanaume ambao wanaweza
kuwaridhisha kitandani na wewe ukawa mwanamke jina tu.
#3 Tabia. Hapa napo kuna tatizo. Wewe mwanaume tabia zako ni
zipi? Huezi tarajia uwe na tabia zinazokera na mimi niwe niko na wewe
tu. Ok, sawa pesa unazo sikatai lakini je, mlo wako ukoje? Uvaaji wako
ni upi? Mazungumzo yako ni ya aina gani? Tabia ulizo nazo kama ni mbaya
hata siwezi kutoka na wewe mbele za watu. Haoa sasa itabidi nikatafute
mwenzako ambaye naweza toka out nae.
#4 Distance. Hii nayo pia huchangia sana wanawake kutokuwa
waaminifu. Mapenzi yamenizidia na wewe uko mbali baba nifanyeje?
Nitavumilia sawa lakini itafika pahali nitashindwa. Rafiki zangu kwa
raha zao na wapenzi wao mimi huku navumilia nitashindwa. Pia hapa si
kila mwanamke si mwaminifu. Kuna wengine ambao wanaweza kuvumilia pia.
Hivyo basi yategemea na mtu mwenyewe. Lakini distance mara nyingi
huvunja mahusiano.
#5 Mawasiliano. Je wewe hutumia muda mwingi kuwasiliana na mpenzi
wako? Waeza pata mwanaume anakaa mwezi mzima bila hata kumjulia hali
mpenzi wake. Mawasiliano ni muhimu sana katika maisha ya wapenzi wawili.
Ukikaa muda mrefu bila hata kutoa sababu ya kimya chako mwanamke
anaweza kufikiria umemuacha.
Haya kazi kwako. Kama unaona unakosea jirekebishe kabla hujapoteza.
Sunday, October 21, 2018
Sababu Zinazowafanya Wanawake Wengi Kuplay Waume Zao
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment