Kuna ishara nyingi ambazo ni vyema tukajifunza ili kuwa makini na
kuchukua hatua pale unapoziona kwa mwanaume. Ni vigumu kukubaliana nazo
lakini ukweli siku zote huwa unabaki palepale lazima tujifunze kama
ifuatavyo:
Kutokujali
Ukiona mwanaume ameacha kabisa kukujali. Tofauti na namna ambavyo
alikuwa mwanzo kwamba atakuuliza umekula, upo wapi ujue kabisa mtu huyo
ameshakutoa moyoni. Kwa mtu unayempenda haiwezekani vitu hivyo vikakata
ghafla na vikadumu kwa muda mrefu.
Mwanaume anakaa wiki moja, mbili na hata mwezi mzima bila kukuuliza
chochote, jiongeze na uanze kuchukua hatua za kumtoa moyoni. Kama mtu
hakujali ni dhahiri hana mpango na wewe, utateseka bure kuendelea
kumuwaza wakati yeye anafurahia maisha ya uhusiano na mtu mwingine.
Mwanaume alikuwa akikupigia simu kila wakati, akikutumia ujumbe kila
wakati lakini ghafla ameacha na anakaa muda wa mwezi au miezi bila
kukupigia wala kukutumia uijumbe wowote, huyo hakutaki. Yeye hawasiliani
na wewe lakini wewe kila uchwao ndiyo unakazana kumpigia.
Mbaya zaidi hata simu zako hapokei, hilo ni tatizo. Si mara moja au mara
mbili unafanya hivyo lakini hajali, tambua kabisa unapoteza muda wako
bure. Mwanaume huyo anakuwa tayari ana mtu mwingine au alichokuwa
anakitafuta kwako ameshakipata au pengine matarajio yake kwako sivyo
alivyotegemea.
Mwingine anakuwa mtu wa kukuita pale tu anapokuwa na matamanio ya
kimwili. Anakuita na baada ya hapo, hazungumzi na wewe tena. Hakupi
ushirikiano wowote hadi pale atakapokuwa anahitaji kuonana na wewe ndipo
anakupigia simu kwa kujifanya anakusalimia ili ukimjibu vizuri, anaomba
muonane faragha.
Tuesday, October 30, 2018
Tabia za Mwanaume Ambaye Hakutaki
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment