Mimi nimekulia mazingira ya kuchungwa sana. Nilikuwa siruhusiwi hata
kujichanganya na watoto wenzangu zaidi ya wa shuleni tu. Hata kukiwa na
birthday ya rafiki yangu wazazi hasa mama hakuwa akiniruhusu. Alikuwa
anadhani sijui nitaharibika au sijui alikuwa kwanini anafanya hivyo.
Sasa kuna kipindi mtoto wa mama yangu mdogo alikuja kukaa nyumbani.
Alikuwa amemaliza form six anasubiria majibu. Kwa wakati huo kulikuwa
hakuna dada wa kazi.
Tukirudi shule baada ya kula kawaida wote tunalala lakini akawa
anawaambia wadogo zangu wao wasilale waende wacheze nje halafu mimi ndio
naambiwa nilale. Kwa njia hiyo akanifanyia anachotaka kunifanyia.
Nakumbuka sikuweza kwenda shule takribani wiki nzima. Niliumww
nikapelekwa hospitali nikapatwa na malaria na dawa nilimeza. Sikuwahi
kuwaambia wazazi wangu, akaendelea na tabia yake hiyo mpaka akaja
kuondoka.
Mara nyingine mtoto wa aunt yangu alinifanyia kitendo kinachofanana na
hiko. Kipindi hiko sisi na aunt yetu tulikuwa tunaishi karibu. Sisi
Tabata Bima aunt yangu anaishi Tabata Alfaruk; sio mbali ziko karibu
karibu.
Nilikuwa standard 7 yeye mtoto wa aunt yangu ambae ni kaka yangu alikuwa
anasoma chuo sijui IFM sikumbuki vizuri. Mama akaniambia niwe naenda
ananifundisha mathematics nilikuwa naenda Ijumaa hadi Jumapili.
Huyu kaka yangu ambae mtoto wa aunt yangu pia akanifanyia anachotaka
kunifanyia. Kuna siku aunt yangu alitukuta tukiwa pamoja alimgombeza
mtoto wake akampiga lakini akanibembeleza nisije kumwambia baba na mama
au mtu mwingne.
Yote yanatokea sikuwahi kumwambia mtu yoyote zaidi ya leo naandika hapa.
Lakini kitu ambacho najiuliza kwanini wazazi wangu walijitajidi sana
kunizuia na watu wa nje ya nyumbani wakasahau kunizuia na watu wa karibu
yangu mpaka nikawahi kufanyiwa mambo ya utuuzima nikiwa na miaka kumi
tu.
Natamani siku niwaulize kwanini waliwaamini sana watu juu yetu sisi
lakini siwezi sababu hawajui sikuwaambia na sitawaambia itabaki siri
yangu. Lakini siku hata nikawa na familia yangu siwezi kuamini mtu
yoyote juu ya watoto wangu
Hili ni funzo sana kwangu!
Friday, October 5, 2018
Home
/
Unlabelled
/
Ushuhuda: Wazazi Wanalinda Watoto Dhidi ya Watu wa nje Wakati Waharibifu Wako Ndani ya Familia
Ushuhuda: Wazazi Wanalinda Watoto Dhidi ya Watu wa nje Wakati Waharibifu Wako Ndani ya Familia
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment