Artikel Terbaru

Responsive Ads Here

Friday, October 26, 2018

Video ya Wizkid na Tiwa Savage yazua gumzo


Video ya wimbo mpya wa msanii maarufu wa Nigeria, Wizkid aliyomshirikisha msanii mwenzake mwanadada Tiwa Savage imezidi kuzua gumzo mtandaoni.

Wimbo huo unaokwenda kwa jina la 'Fever' uliachiwa rasmi Jumanne, Oktoba 23 katika mtandao wa Youtube, ambapo mpaka sasa ina watazamaji zaidi ya 435,000.

Mashabiki mbalimbali wa muziki katika mtandao wa Twitter wameonesha hisia tofauti juu ya wimbo huo hasa kutokana na kitendo cha Wizkid kumtumia Tiwa Savage kama 'Video Vixen" katika wimbo huo.

Pia kuvuma kwa video hiyo kumechangiwa na tetesi za hivi karibuni kuwa wawili hao wana mahusiano ya kimapenzi, jambo ambalo limewafanya wengi miongoni mwa mashabiki kuamini baada ya kuitazama.

@Emmanuel aliandika, "Wizkid ana mahusiano na Tiwa Savage?. Video hii ina mengi ya kutueleza".

@Newscantell naye alichangia mjadala huo kwa kuandika, "Japo hatusemi kuwa Wizkid ana mahusiano na Tiwa Savage ama la, lakini acha tuwe wakweli, kwa video hii ni kielelezo tosha".

@Missyayom ameandika, "Hakuna chochote kitakachonifanya niamini kuwa Tiwa Savage na Wizkid wana mahusiano, hawa wawili wanatuigizia. Wanatupatia kile tunachokihitaji".

Ikumbukwe kuwa mwanadada Tiwa Savage aliolewa na Tunji "Tee Billz" Balogun, 23 Novemba 2013 kabla ya kutengana mwaka 2016. Kwa pamoja walifanikiwa kupata mtoto mmoja aitwaye, Jamil mwaka

No comments:

Post a Comment