Sio Kila EX wako anayeomba Mrudiane anamaanisha! Wengine huomba kurudi
ili wakutesti tu jinsi ulivyo Mbulula,jinsi usivyo na msimamo na jinsi
ulivyo CHEAP na huna Misimamo wala Future.
Jitu mmeachana miezi 6,leo linakutesti lirudishe majeshi,na wewe ulivyo
kiazi,upo-upo tu,ina maana miezi yote hii ulikuwa umeganda unasubiria
rehema zake ama??
Kurudia Matapishi ya EX ukitegemea Amebadilika ni Sawa na Kupika Sufuria la Makande kwa Mshumaa,Utaambulia Masizi tu..
Kipi kipya kakiona kwako hadi arudi??Nini Kilimshinda huko nyuma ambacho leo anakiweza anataka kurudi??Akafie Mbele huko.
KUWA NA MSIMAMO,Ukisema Its Over umaanishe,sio unakuwa na hisia
zinapepea tu kama Bendera ya Katibu Kata wa Kishumundu...Mtu kama
Hajielewi achana nae,siku akijirudisha mwambie kwanza akapimwe Minyoo ya
Kinyarwanda.
Umekazana kuwaambia marafiki zako 'Siku hizi hakuna Mapenzi ya dhati
watu wote Majanga tu',nani amekwambia hayapo??Yapo sana ila wewe
unatumia mbinu tofauti..Huwezi kusoma Degree ya Law halafu u-apply kazi
ya Chief Accountant wa Bodi ya Tumbaku...Kila siku utasingizia Balance
Sheet haina Jurisprudence..Lawyers mmenielewa!
Acha kudate watu wasiojielewa,Usidate kwa sababu uko lonely,Usiwe
desperate kuingia Mahusiano kwa sababu shosti zako wanakusimulia
walivyopelekwa Ruwenzori Waterfalls..Ingia kwenye Mahusiano pale Moyo
wako ukiwa tayari na mtu uliyemfia kihisia na amekuwa approved na
Veins,Auricles,na Aorta za Moyo wako kwamba He/She is really the One..
Unadate na mtu ambaye mustakabali wake mwenyewe haujui,ukimuuliza
anataka kuwa wapi ndani ya miaka 5 ijayo anakwambia Mungu anajua dont
worry,halafu BBM na Instagram unajiita Baby Ake Mie Iam in
Love..Utaishia kufua boxer hadi kucha zinukie gololi!
Mbwa kamwe hashughuliki na kesi za Paka kufungiwa kabatini.Date the
Right Person,With Right reasons,in a Right Time uone kama Mapenzi
hayapo...
Friday, November 16, 2018
Akina Dada, Sio Kila Ex Wako Anayeomba Mrudiane Anamaanisha...
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment