Katika mahusiano mwanamke anakua anahitaji mambo mbalimbali lakini si
yote atakua anamwambia mpenzi wake au mume wake. Kichwani mwake anajua
kama unampenda basi vitu hivyo hautavisahau.
Sasa hapa ndugu zangu wanaume inapasa kuchekecha akili na kujiongeza kwa
maana vitu hivi huwa vinasaidia kuendelea kuwaweka karibu katika
mahusiano.
Leo tutaangalia baadhi ya vitu ambavyo mwanamke/mke anavihitaji kutoka kwa mwanaume/mme wake..
1. Kutomuonesha mfumo Dume, sio lazima kwenye kila jambo basi uwe
unaweka na kutanguliza mfumo dume. Siku nyingine jishushe kwa
mkeo/mwanamke wako itasaidia kumvuta karibu na kuongeza mapenzi kwako.
2. Mpe sikio, hakikisha unamsikiliza mke wako anapokua anakueleza jambo.
Na hapa unatakiwa umsikilize kwa makini akiwa anakueleza mambo ya
msingi na mambo ya utani pia. Muda mwingine mwanamke anahitaji
kusikilizwa tu roho yake inatulia.
3. Zawadi, mwanamke anapenda kupewa zawadi hivyo ni vema ukawa na
utaratibu wa kumpa zawadi mke wako hata kama ni vitu vidogo vidogo kama
maua, choklet, Ice cream, kutoka nae mtoko n.k
4. Mpambe kwa sifa, kwa walio kwenye mahusiano wanajua ladha ya kusifiwa
na mpenzi wako. Mwanamke anahitaji umsifie kwa uzuri na mambo yake
mengine. Hii ikibidi kila siku uwe unamsifia basi hauna budi kufanya
hivyo.
5. Kumjulia hali mara kwa mara, mwanamke anapenda kujuliwa hali na
kutafutwa mara kwa mara na mpenzi wake. Hivyo ni vema ukawa na utaratibu
wa kumtafuta hata kwa kumtumia ujumbe mfupi au kumpigia hata kama upo
kazini kwani haihitaji muda kumtumia mkeo ujumbe kumjulia hali. Hii
itasaidia mwanamke aone unamjali na unampa kipaumbele katika maisha
yako.
6. Mshukuru, uwe na utaratibu wa kumshukuru mke wako hata kwa mambo
madogo madogo usisubiri mpaka afanye jambo kubwa au ukumbwe na matatizo
akusaidie ndio umshukuru. Unaweza ukamshukuru kwa kukupikia, kukufulia,
kulea watoto vizuri n.k
Kama nilivyoeleza hapo awali hayo ni baadhi tu ya mambo ambayo mwanamke anayahitaji lakini hawezi kumwambia mwanaume ampatie…
No comments:
Post a Comment