Umewahi kufikiria faida zinazopatikana kwa kumkumbatia mkeo mkiwa
mmelala? Famasia yako ya Ndoa Maridhawa inakuletea faida 6 za
kukumbatiana kitandani:
1. HUPUNGUZA SHINIKIZO LA KISAIKOLOJIA:
Unapomkumbatia mkeo mkiwa mmelala husaidia kuzalisha kichocheo (homoni)
cha furaha kiitwacho oxytocin. Homoni hii hufanya kazi ya kupunguza
hatari ya kupatwa na maradhi ya moyo na kupunguza shinikizo la
kisaikolojia. Hilo pia hupelekea kupunguza hatari ya kupatwa na maumivu
ya kichwa na maradhi mengine.
2. USINGIZI MARIDHAWA:
Wanandoa wanapokumbatiana husaidia kulala vizuri. Tafiti mpya zimeonesha
kuwa kumbatio hupunguza cortisol na hivyo kupunguza shinikizo la
kisaikolojia. Pindi cortisol inapopungua mwilini, moja kwa moja usingizi
huwa mzuri na mwanana.
3. Unapomkumbatia inaweza kusababisha raha, hasa mambo yanapofikia
kwenye hatua ya kucheza, lakini kabla ya hapo furahia ladha ya mgusano
wa ngozi zenu kabla ya kusonga mbele… Moyo wako unatakiwa kuuhudhurisha
katika eneo na muda wa mgusano huo ili kujenga uaminifu na hisia za
ushirika.
4. Kukumbatiana huwapa fursa ya kuwasiliana bila kuongea. Na hili ni jambo maridhawa kabisa kwa wanandoa kuzidi kuwa karibu.
5. NI DAWA YA FADHAA:
Kimbilia kitandani. Kumbuka kuwa kitanda kipo kwa ajili hiyo. Achana na
kitabu, televisheni, simu, tablet na mambo mengine kama hayo. Kumbatio
litakusaidia kumakinika na kupata utulivu.
6. HUWAPA HISIA ZA KURIDHIANA NA KUTOSHEKA:
Mnapokumbatiana bila kuwa na lengo la kuingia kwneye tendo la ndoa,
mtapata hisia kubwa ya kuridhika na ndoa yenu. Tafiti mbalimbali
zimeonesha kuwa wanandoa wanaokumbatiana wanaridhika sana na ndoa zao
kuliko wale wasiokumbatiana
No comments:
Post a Comment