Kukosea katika uhusiano ni kawaida kabisa, naweza kusema ni sehemu ya
maisha, lakini pia ni vizuri kuhakikisha kuwa unakuwa makini ili
usikosee kila wakati.
Hata hivyo, inawezekana kuwa makini na kujitahidi kutomuudhi mpenzi
wako. Hilo linawezekana ikiwa utakuwa makini na kutambua mpenzi wako
anapenda vitu gani na anachukia vitu gani.
Baada ya kufahamu kuwa jambo fulani halipendi, ni vizuri ukaacha kabisa
kutumia kauli hizo mbaya ambazo kwa namna moja ama nyingine zinaweza
kukusababisha kukosana na mpenzi wako, hivyo kusababisha doa katika
penzi lenu.
Kuna baadhi ya watu wakiwakosea wapenzi wao, si wepesi kukubali makosa
na kuomba radhi, badala yake huendelea kuwa wakatili wasiotaka ushauri
wa aina yoyote. Hayo ni makosa.
MAKOSA YAMEHALALISHWA?
Hapana! Hayajahalalishwa ila ijulikane wazi kuwa makosa katika maisha ni
hali ya kawaida kabisa, usishangae kuwa na makosa katika uhusiano ni
hali ya kawaida ambayo huweza kutokea si tu katika uhusiano bali hata
maisha ya kila siku.
NINI CHA KUFANYA?
Hapa naweza kusema kuwa ndiyo penye mhimili wa mada yetu ya leo, kwakuwa
kukosana ni jambo la kawaida katika uhusiano, basi lazima ifahamike
jambo mbadala la kufanya baada ya kutokea mtafaruku katika uhusiano.
Ikitokea umemkosea mpenzi wako na ukajua wazi kuwa ni kweli umemkoesea,
ni wajibu wako kumuomba msamaha. Hata kama wewe ni mwanamume, kwa sababu
wanaume hujiona wao kuwa ni vidume kwa hiyo hawaoni sababu ya kuomba
msamaha pindi wanapowakosea wapenzi wao.
Naweza kusema huo ni ulimbukeni usio na maana, kwani kusema samahani
utapungua wapi ndugu zangu? Sema nisamehe mpenzi wangu ni hali ya
kawaida, nilipitiwa kidogo!
Bila shaka mpenzi wako atakuelewa na kukusamehe na maisha yataendelea
kama kawaida. Usijijengee ujeuri katika mapenzi, huna jeuri yoyote
katika mapenzi, kwani ukifanya jeuri itasaidia nini katika maisha yako?
Hata kama wewe ni mzuri sana, lakini unatakiwa kutambua nafasi yako kwa mpenzi na nafasi ya mpenzi wako kwako.
Tumia kauli nzuri na umfanye atambue kuwa hukufanya makusudi bali
ulimkosea kwa bahati mbaya. Onesha jinsi unavyojuta kutokana na wewe
kumkosea, bila shaka baada ya kugundua kuwa ulimkosea kwa bahati mbaya
lazima atakusamehe.
KAULI CHAFU AU NJEMA?
Hapa kuna jambo jipya kidogo, inawezekana kwa kuwa wewe ndiye
uliyekosewa na mpenzi au wewe ndio mkosaji, ukatatizika na aina ya kauli
inayokupasa kuitumia kwa ajili ya mpenzi wako na mkafikia mwafaka mzuri
wa kupendeza.
Hata kama wewe ndiye umekosewa huruhusiwi kabisa kutumia kauli
chafu/kali kumweleza mpenzi wako jinsi ulivyochukia, badala yake
unatakiwa kuwa mtulivu na kauli nzuri mbele ya mpenzi wako.
Mweleweshe kwa upole, tena ukitumia kauli ya upole inakuwa rahisi
kukuelewa na kuomba radhi, hali itakayorudisha maelewano baina yenu.
Pamoja na hayo yote unyenyekevu wakati wa kuombana msamaha unahitajika
sana, ni vizuri kuwa na unyenyekevu na utulivu wa hali ya juu wakati
unapomwomba msamaha mpenzi wako ili mambo yaweze kwenda sawa.
Ni vizuri wapenzi kuwa na kauli nzuri inapotokea kuhitilafiana, mkumbuke kuwa kukosana ni kama sehemu ya mapenzi.
Epuka kuwa na hasira sana wakati wa kuzungumza juu ya tofauti zenu.
Maneno makali ya kuropokeana si mazuri kabisa wakati mnawekana sawa,
kauli njema zitumike ili mambo yaweze kuisha bila kusababisha matatizo
mengine mapya.
Suala la kukoseana katika maisha ni jambo la kawaida, si hivyo tu bali
hata katika uhusiano. Lazima tukubali kuwa makosa yapo, mpenzio
anapokukosea isiwe jambo la kushangaza sana, tambua kuwa ni hali ya
kawaida ambayo unatakiwa kuikubali kwa hali yoyote.
Kuwa na moyo wa kusamehe pindi mpenzi wako anapokukosea na kukuomba
msamaha. Tambua kuwa anakuomba msamaha kwakuwa anatambua kuwa alifanya
makosa na hakufanya kwa makusudi.
Kubwa zaidi ambalo linapaswa kuzingatiwa ni kwamba utakapomkosea mpenzio na kumuomba radhi, basi hakikisha kuwa hurudii makosa.
Tuesday, November 20, 2018
Jinsi kauli yako inavyoweza kugharimu penzi lako
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment