Najuta ni kiherehere cha moyo wangu kukupenda,kukuthamini na jukujali.
Naombeni msaada,ni mpenzi wangu yapata 1&half year katika mahusiano ni binti ambaye tulifahamiana nae siku moja alipokuja na mama yake mdogo ofisini kwangu kupata huduma,
huyu mama yake mdogo ni mtu ninaefahamiana nae hivyo basi akaona haina budi kunitambulisha kwa mwanae nami nikaona ni vizuri kuanzia hapo binti yule alianza kunizoea na kuonesha dalili zote za kunitaka hata baadhi ya siku hufunga safari na kuja kunisalimia.
nami sikua na hiyana huwa sipendi kumkwaza mtu nikawa nampa ushirikiano tu mzur.
kutokana na ubize wa kazi yangu muda wa story huwa sina nikamwambia kama hutojali uwe unakuja saa 12jioni muda ambao nipo off ila sijui kama mama yako mdogo atakubali akasema hilo halina shida nikimwambia nakuja kwako hawezi kunikatalia kiukweli hilo jibu lake lilinipa ulakini!!
Basi jioni tukawa tunaenda sehemu ya utulivu tunapiga story sana tunapata chakula then tunaondoka tuliendelea hivyo kwa muda mrefu huwa anakuwa kama na kitu cha kutaka kuniambia lakini anashindwa kila usiku lazima anipigie simu na asubuhi lazima aniulize umeamkaje.
kutokana na tabia zake nzuri alizozionesha kwangu nikaona pengine Mungu ndo kanionesha mke mwema nikamtongoza japo sikutumia nguvu hata kidogo alitabasam na kufurahi nakumbuka alinikumbatia na kunipiga busu hadi nilihisi kuwewesuka kwa joto lake.
Nikawa namhudumia kila alichokitaka nilimpatia na alinipenda na kuniheshimu kama mume wake.
Nakumbuka aligombana na mama yake mdogo akawa kahamia kwa dada yake ni mbali kidogo huko nadhani maisha yalikuwa ya shida,alikuwa akinipigia simu "leo baby sijala"nikawa namsaidia akiugua namtumia pesa za matibabu,
SASA basi miezi miwili imepita kapata kazi basi ni dharau mwanzo mwisho simu hapigi,text hanitumii hata nikimtext baada ya masaa mawili ndo anareply tena shortly wiki tatu zimepita kanipigia simu anaumwa bila hiyana nikaenda kumuona na nilimpa kila kitu anachohitaji mgonjwa sikutaka maongezi nikaondoka zangu hadi leo sijawasiliana nae sababu ninahasira nae sana na ninataka nimfanyie kitu ambacho hatakisahau ili iwe fundisho au nyie wanajamvi mnanishauri nini?
No comments:
Post a Comment