Kina mama wenye mimba ambao huongezeka uzito kwa kasi katika miezi
mitatu ya mwanzo ya ujauzito wanakabiliwa na hatari ya kupata kisukari
cha mimba (gestational diabetes). Kifafa cha mimba ni hali ambayo
wanawake ambao huko nyuma hawakuwa na ugonjwa wa kisukari huonekana kuwa
na ongezeko la sukari katika damu kwa mara ya kwanza wakati wa
ujauzito. Kwa mujibu wa uchunguzi mpya, mama wajawazito ambao wataongeza
uzito wa gramu 403.70 kwa wiki wako katika hatari ya kupata kisukari
cha ujauzito zaidi ikilinanishwa na wale watakaoongeza uzito wa chini ya
gramu 272.15 kwa wiki. Bi. Monique Hedderson aliyeongoza uchunguzi huo
amesema kuwa, ongezeko kubwa la mafuta ya mama mwanzoni mwa mimba
kunaweza kukaathiri kwa kiasi kikubwa tishu za mwili na kuzifanya
zisikubali insulin, jambo ambalo taratibu husababisha kisukari cha
ujauzito. Kwa ajili hiyo wataalamu wameshauri kwamba, wakina mama wenye
mimba hasa wale wanene na wenye uzito mkubwa wanapaswa wajiepushe na
kuongezeka uzito mwanzoni mwa mimba ili wasipwatwe na kisukari cha
mimba.
Sio vibaya kutambua kwamba, asilimia 4 ya kina mama ambao watapata kisukari wakati wa ujauzito wanakabiliwa na hatari ya kupata ugonjwa wa kisukari baadaye maishani mwao, hiyo ikiwa ni pamoja na watoto wao. Kisukari cha ujauzito kina dalili kadhaa lakini kwa kawaida huainishwa kwa vipimo (screening) vinavyochukuliwa wakati wa ujauzito.

No comments:
Post a Comment