Kijana anayedaiwa kuzaa na msichana wa kazi aliyedai mwanaye wa miezi
mitano alikuwa akifungiwa kabatini na mwajiri wake tangu alipozaliwa,
amekamatwa na polisi mkoani Dodoma.
Kijana huyo, Salum Waziri, amekamatwa baada ya agizo lililotolewa na mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi.
Katambi alisema Waziri amekamatwa kwa tuhuma za kumpa ujauzito Neema
Matimbe ambaye ana miaka 15, ambaye alikuwa mfanyakazi wa ndani wa
mwalimu, Anitha Kimako.
Alisema pamoja na tuhuma zinazomkabili Anitha kuwa alimfungia kabatini
mtoto wa binti huyo, kulikuwa na ulazima wa kumsaka kwanza baba mzazi wa
mtoto yuko kwa sababu alifanya kitendo hicho kwa binti mwenye umri
chini ya miaka 18.
Katambi alisema kijana huyo ni mkazi wa Area C alikataa mimba ya mtoto huyo.
Kaimu kamanda wa polisi wa mkoa, William Mkonda alisema kijana huyo
atafikishwa mahakamani muda wowote uchunguzi utakapokamilika.
Wednesday, January 16, 2019
Home
/
Unlabelled
/
Mwanaume Aliyempa Mimba Binti wa Miaka 15 Mama Mtoto Aliyefungiwa Kabatini Atiwa Mbaroni
Mwanaume Aliyempa Mimba Binti wa Miaka 15 Mama Mtoto Aliyefungiwa Kabatini Atiwa Mbaroni
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment