Tukiwa
sebuleni nilianza kumueleza Getruda. Moyo uliniuma kila nilipo kumbuka
aliyonifanyia “Mke wangu kama ingenipasa kusema, nini kinacho ikera
nafsi yangu ni kuni dhalilisha ndani ya kadamnasi, sio wafanyakazi wangu
wa wageni, wote wanafahamu ulilolifanya, na isitoshe ile ni hotel yangu
unadiriki kufanya mapenzi ukitoa kashfa ili kuinufaisha jamii, kumbuka
aibu si yangu pekee, ni yetu wote.”
Sijui
ni mkate sikio au nimpe kilema kwenye via vya uzazi ni mchome na moto
wa umeme (hita)asiweze kufanya tendo la ndoa maisha?.Ndio itakuwa
fundisho,kiherehere kitamuisha”wakati na waza cha kumfanyia, nilikatishwa na sauti.
“Mume
wangu kumbuka wewe ndio uliyenitafutia mwanaume wa kuniridhisha
kimapenzi, ilinijisikie nina mume, basi kama ni hivyo nami sitaki penzi
la mtu mwingine wa nje. Nataka penzi lako nilikubali kwa kukuheshimu.
Mwanamke kawaida hatafutiwi mume, anatafuta mwenyewe, hisia zote
nilizoweka kama nipo na wewe, iweje useme na kudhalilisha, kama
utashindwa leo kesho nataka talaka yangu,asubuhi na mapema,
umenielewa?”Getrudaalinisemesha kwa ukali.
“Sio
nimekukataza usiwe naye, kinachonikera ni kunidhalilisha na kutoa siri
ya unyumba wetu, sina wivu na mapenzi yako.Ninachotaka unihifadhie siri
moyoni mwako”niliinamisha kichwa chini kama kobe.
“Mume wangu nakutunzia heshima kuliko mtu yeyote duniani, nashangaa!unapo sema nainfaisha jamii.
Kama angekuwa msichana mwingine asinge vumilia hata wiki moja, na
washukuru wazazi kunifundisha uvumilivu ndani ya nyumba”Aliendelea
kuongea,asijue nina mawazo nini moyoni.
Tukiwa
kwenye mazungumzo,nilisikia simu ikiita,nilijipapasa kama ilikuwa simu
yangu.Nilipotizama pembeni nilimuona Getruda akitoa simu yake kwenye
pochi ndogo ya rangi nyeusi iliyojaa nakishi nyingi.
“Hallo,
uko wapi?”Getruda alipokea tu,baada ya kuona jina juu ya kioo cha
simu.Niligutuka nikahisi mtu huyo anamfahamu,ndio maana alimuuliza
aliko.
“Aaaa..nipo Makutano bar hapa napata moja baridi moja moto.Vipi mume bwege yupo?”
“Yupo
anakusalimia”Getruda alisema na kunitupia jicho ,akacheka kidogo na
kuendelea, “Utakuja kutusalimia?”Getruda aliongea akiniongoa wasi wasi.
“Ninani huyo unaongea naye?”Nilijikuta nikisema wakati Getruda anaongea na simu.
“Wivu
umekuzidi mume wangu.Kila kitu unataka kujua hebu chukua basi uongee
naye”Getruda aliibadilikia kwa ghafla,alinyoosha mkono wake
akitakakunikabidhi simu.
“Sihitaji kuongea nae,nimekuuliza kwani vibaya?.Nilifikiri ni mama amekupigia simu”
“Hapana.Nirafiki yangu”Kisha akaendelea kuongea nae.
“Samahani kwa usumbufu uliojitokeza.Mume wangu anwivu ilembaya”
“Sasa wivu wanini wakati hayawezi?”Sauti nzito upande wa pli ilisikika ikisema.
“Hata mimi nashangaa!”Getruda alidakia na kuangua kicheko kikubwa.
“Mpenzi sikia…..naomba ufike sasa hivi hapa Makutano bar”
“Mama
anaumwa sana!.Ehhe mmempeleka hospitali?”Getruda aliongea maneno hayo
akiwa tayari kesha kata simu.Aliendelea kuongea simu ikiwa imekatika
ilimradi anipumbaze “Ana umwa na nini hasa?” alitulia sekunde mbili hivi
akaendelea, “Ooo! My god .Kuna uwezekana wa kupona?”
alitulia tena sekunde kadhaa hivi, “Sawa.Ninakuja sasa hivi huko”Akajidai kukata simu.
“Vipi mbona jasho linakutoka?.Mama anaumwa na nini?”
Nilimwuliza
sekunde chache alipokata simu. “Mama alidondoka ngazi akiingia
kanisani”Getruda aliongea kiupole kabisa, akionekana kujizuia kulia.
“Kanisani?”
“Ndio.Na hivi sasa yupo amepelekwa hospitali ya Kcmc kwa matibabu” Safari hii alifura na alifanya kulalamika chini chini.
“Ooo! Pole sana mke wangu.Unaonaje nikaoga tukaenda wote?”
“Utanichelewesha sana”
“Basi siogi tena. Ngoja nivae twende,tena nina siku nyingi sijaenda kumsalimu”Niliongea nikiamka kitini, tayari kwa safari.
“Hapana.Nitakuletea taarifa ya hali yake.Nyumba tutamuachia nani?”
“Hilo halina shida.Nisubiri”
“Sitaki
bwana. Wee kila mahali unataka kuongozana na mimi.Nimeshachoka, ngoja
niende kisha kesho nikirudi nitakuja kukuchukua kwani hata kupajua
hupajui.Unapafahamu pale tulipokuwa tukiishi zamani” Nilisimama kama
mlingoti ,nikavuta pumzi na kuzishusha kwa nguvu.Nikatikisa kichwa na
kusema “Sawa.Kama hutaki nikapajua kwenu leo ….hata kesho nitapajua”
Niliona
Getruda akitoa tabasamu kubwa ,hakuishia hapo alinifuata nakunibusu
shavuni “Mwaaaa”Kisha akaokota kipima joto chake,na kutoka kwa haraka
akionekana mwenye wasi wasi mkubwa.Alipofika mlangoni aligeuka na
kunitizama kama akinihurumia vile,sikugundua kitu ,nilibaki
nimeduwaa.Akanipungia mkono na kusema “Bye bye”Nami nikapunga kono langu zito kigoigoi bila tabasamu.
Getruda
alimpigia simu mteja wetu wa kila siku katika usafi,si mwingine bali
Jangala. “HalloJangala tafadhali naomba unichukue hapa nyumbani”alisema
baada ya simu kupokelewa.
“Sawa.Namshusha abiria hapa mjini nakuja”
“Ok”Alijibu na kukata simu.
Kama kawaida yake Jangala huwa hakaidi na hana tamaa.Aliingia na kusimama mbele ya Getruda binti Kimario.
“Shem vipi.Wapi leo pa kula kuku.Si unaelewa wiki end”Jangala alimtania Getruda.
“Ndio.
Wiki end lakini kwangu imenijia vibaya .Nimepata taarifa mama yangu
mgonjwa.Naomba unifikishe karibu na Makutano bar nikampe taarifa
shangazi yangu.Kisha utaendelea na safari yako.Mimi nitakupigia kama
nitakuhitaji tena”Getruda alidanganya.
“Sawa.Riziki ndogo ndogo hizi usininyime shem.Pole sana kwa kuuguliwa na mama yako”
“Nishapoa shem”Alimjibu kiunyonge.Getruda hakuuguliwa wala nini.Alipokuwa akienda ni Makutano bar kukutana na Mzee Jophu Kundy.
Katika mazungumzo yao walijikuta kufika Makutano bar, “Tafadhali nishushe hapa.Kuna uchochoro gari haliwezi kuingia huko.Shilingi ngapi?”
“Elfu nne zinatosha shem”Jangala alisema akimtizama Getruda.
“Punguza shem.Hujui mimi mteja wako?”
“Petroli imepanda bei sana shem. ‘Any way’ nipe tatu unusu”Jangala alisema .
Getruda alimpatia Jangala elfu tatu na mia tano,akashuka garini.
“Usihaike shem.Nitafunga mwenyewe mlango.Mteja kwangu ni
mtukufu”Jangala alisema baada ya kumuona Getruda anataka kufunga mlango.
Getruda alijidai kama anaingia uchochoroni ili Jangala aondoke
zake.Alipogeuka aliona gari la Jangala likiishia bali kabisa.Aligeuka na
kurudim kuelekea kule Makutano bar.
*****************
Ndani
ya makutano bar,alionekana mwanaume wa makamo.Kwa kumtizama ungeweza
kukisia anamiaka hamsini ama hamsini na tano.Kichwa chake kilikuwa na
mvi za kuhesabika.Uso wake ulisha anza kuwa na makunyanzi ya uzee.Alivaa
suti ya kahawia,na viatu vya pembe nne ‘Four angile’.Shingoni alinyonga
tai ya bluu iliyozidi kumfanya maridadi.Mkononi alivaa saa ya seiko 5
ya dhahabu.Meza aliyoketi ilijaa vyakula na vinywaji.
Mara
kwa mara aliinua mkono wake wa kushoto akitizama muda,alipomaliza
aligugubia glasi ya bia mdomoni na kuirudishia glasimezani.Pia muda wa
kuiacha pombe ishuke vema tumboni alitupa macho yake lako la kuingilia
wateja.Safari hii ilikuwa mara ya kumi kutizama lango hilo,alipohamisha
macho aliyapeleka kwenye glasi ya kinywaji,akaona kama bia ilishaisha
glasini,alikamata chupa ya bia na kumimina kiasi kwenye glasi ya
bia.Hakuchelea aligugubia kama mikupuo miwili bila kuishusha
mezani,alipomaliza akacheua kama mara tatu hivi,alihisi kilevi kikipanda
vema ndani ya ubongo.Akajikuta akicheka mwenyewe
“Mimi ndiye.Mwingine hakuna”Alisema nakutizama simu yake.Aliiokota nakujaribu kupiga,simu aliyopiga iliita bila kupokelewa.
“Shiit.Kwanini hapokei?”alipayuka kwa ghadhabu.
Hakuchoka akapiga mara ya pli,iliita tena,akasikia ikipokelewa “Hallo Prety girl.Uko wapi mbona hupokei simu yangu?”
“Nakaribia jengo la Makutano hapa”
“Sawa.
Nakusubiri kwa hamu wa moyo”Walikata simu.Mzee Jophu akawa habandui
macho lango la kuingilia,alitaka kumwona Getruda akiingia kwa
madaha.Ghafla aliona mlimbwende akiingia kwa mapana na kumfanya kila
aliyeko mle ndani kumtupia jicho.Getruda hakuwa mzuri sana wa
sura,lakini umbo lake na makalio ndio kichochezi kwa wanaume rijali.Kila
alipovuta hatua ,makalio yake yalitikisika mithili ya mawimbi
baharini.Nafiki jambo hilo ndilo lililomfanya Mzee Jophu ammezee mate
mke wangu.Si kwamba na msifia kwa vile ni mke wangu,hapana.Njoo kwangu
Arusha ushuhudie, ukweli wangu.Lakini kwa sasa ni mzee sana.
“Kaaaa,
kakaka!”alionekana kijana mmja aliyeko nyuma ya mzee Jophu
akihamaki,mfdomo ukiwa wazi kwa mshangao na mkono ukiwa umeshika mdomo wa chini,Jicho likiwa limemtoka kama ndulele iliyoiva.
“Mkindu wavona ilo ibora ledha aho”Kijana huyu alimwambia mwenzake kwa kilugha.
Akimaanisha “Mkindu umeona lisichana hilo linalo kuja hapo?”
“Nikirumo ilo!”Mkindu alijibu.
“Hilo ni balaa!” Wakacheka.
Mzee Jophu alimsindikiza Getruda kwa macho ya matamanio hadi alipomkaribia kabisa.
“Vipi.Mbona umechelewa ?”
“Mume bwege alikuwa akinichelewesha”Getruda aliongea akivuta kiti kilicho wazi.
“Achana nae.Ukisha mkabidhi fisi bucha unamatarajio gani?”
“Kuokota mifupa”Getruda alidakia.
“Hakuna kinachobaki.Fisi gani anakuachia mfupa!”Wakacheka na kupigana mabusu.Kisha akagonga meza.
“Muhudumuuu”aliita.
“Nakuja”sauti ilisikika kwa mbali kidogo.
“Kuja
haraka.Watu wanapesa zao hazina pakwenda”Alisema akijiamini
kabisa.Getruda alimtizama akagundua mzee Jophu alishaanza kulewa.
“Mpati wa moyo wangu kinywaji chochote anachotaka upesi”Muhudumu akaitikia sawa.
“Dada nikupatie kinywaji gani?”
“Henken ya kopo.Usisahau mrija tafadhali”
“Ya baridi au moto?”
“Aaaa! Vuguvugu.Nitapata?”
“Usihofu,utapata”Muhudumu aliondoka.
“Mpenzi
nimekuita nina jambo muhimu la kukueleza,hivyo basi naomba
uwemsikivu”Alitulia kidogo na kuokota glasi ya bia,hakuchelewa alimimina
bia yote na kurudisha glasi tupu.Akacheua mara mbili nakuendelea
“Kwanza kabla ya yote. Napenda unihakikishie kwamba unanipenda”
“Nakupenda sana mpenzi inamaana hujagundua bado?”
“Ninyi wanawake mnabadilika sana.Lazima kila tunapokutana tuulizane jambo hili”
“Si
wote bwana.Unajua ninyi wanaume mkionyeshewa kama mnapendwa sana vichwa
huvimba na kujiona mna matilaba ya kufanya lolote juu ya mwanamke”
“Ni
baadhi ,si mimi Jophu”Akasema na kusogeza kiti jirani na Getruda.Kabla
hajaendelea tayari vinywaji vililetwa,Henken ya Getruda na safari ya
Mzee Jophu.
“Karibuni”Muhudumu alisema.
“Ahsante”Getruda akajibu.
“Wee binti mwite mchoma nyama tafadhali”Hakukawia kufika mchoma nyama. “Kata nyama ya kidari,ile laini…umeelewa?”
“Ndio,bosi”
“Haya futikaa”Alisema kiulevi ulevi.Akamgeukia Getruda, “Wife,sasa tuendelee na mazungumzo yetu”
“Kama umenidhihirishia unanipenda utakuwa upande wangu kwa lolote lile,si ndivyo”
“Ndivyo”
“Nikisema kitu kwa manufaa yetu lazima tusaidiane,sivyo?”
“Ndivyo”alijibu
kiupole hakujua ni jambo gani anataka kuelezwa wakati huo.Kwa sasa Mzee
Jophu akapunguza sauti akamweleza Getruda kwa sauti ya chini
kabisa.Nafikiri alihofu watu kung’amua maneno yake.
“Getruda naomba iwe siri kubwa sana.Nataka tumuondoe Sweedy Duniani”Getruda alishituka sana kama aliyeamshwa usingizini. “Heee!”
“Usishituke
laazizi wangu.Nimeamua hivyo kwa manufaa yetu pia.Kila siku kujiiba
iiba ,tutajiiba mpaka lini?.Heri afe tupate uhuru….”
“Haiwezekani Jophu.Unajua dhambi ya kuua lakini?”Getruda aliuliza.
“Acha ujinga, nani kakuambia kuna dhambi.Nani aliyeenda akarudi akasema kuna adhabu kali?.Niambie”
“Kwenye maandiko takatifu,maneno hayo yapo.”Getruda alijibu akimtizama Jophu.
“Kumbe nimaandiko yaliyotungwa kama hadithi tu.Nitajie nani alikufa akafufuka na kutuonyeshea adhabu alizopata ahera?”
“Bwana acha mizengwe yako.Uhusiano wetu hauwezi kuzuilika kwa sababu ya Sweedy”
“Nitakupa
chochote lakini tumuue Sweedy.Uko tayari?”Getruda alikaa kimya,safari
hii alishindwa kijibu. “Nijibu basi?”Mzee Jophu alimhimiza.
“Nikujibu nini?”
“Kwani
hujui.Sina jibu lolote.”Akamtizama Mzee Jophu ,na kuvutakumbukumbu ya
siku ya kwanza tulipokuwa kanisani,alikumbuka maneno mengi ya
mchungaji.Akanikumbuka nilipompiga busu la kwanza nikiwa namvisha pete
ya ndoa.Pia akakumbuka maneno ya mama yake akimweleza juu ya unyumba
wetu.Machozi yakamtiririka mashavuni bila kujijua.Akapandisha mkono wa
kuume ulioshika leso na kujifuta. Mzee Jophu alinyoosha mkono na
kumpatia funguo Getruda.
“Kuanzia dakika hii.Land cruiser iliyoko nje ni mali yako.”Getruda alishangaa hakuamini kile alichokuwa akikiona wakati huo.
“Mpenzi ni kweli ama ni mipombe inakusumbua akili?”
“Sijalewa
wa moyo.Ninachohitaji sasa hivi, ni kutoa uhai wa huyu hanithi”Akatulia
kama nukta tano hivi ,kisha akasema,“Sawa sawa?”
“Sawa”Getruda
alijibu mapigo ya moyo yakimwenda mbio.Alifikiri na kuona kwanza
alishachoka kukodi teksi kila siku.Naye alitaka kutembelea gari la
kifahari.Alitamani akawatambishie mabinti wenziye aliosoma nao pale Mkuu
Rombo.Watajuaje kwamba naye nitajiri pasipo kutembea na gari la
kifahari?.Aliamini mtu akiwa na pesa huheshimika kuliko hata kitu
chochote duniani.Akajikuta moyo ukipamba na furaha kali, “Acha afe bwana
kwani nini bwana. Mtu kama furushi la nguo, heri afe , wangapi wameuawa
na kuwaacha wake zao na mapesa kibao.Mungu nisamehe”aliwaza akilini.
Waliendelea kunywa na kula nyama choma pale.Getruda alimaliza bia
yake na kuongezwa zingine mbili,tayari ubongo ukafa ganzi.Alianza
kuongea sana,tena bila kujali kwamba alisikiwa na watu. “Mpenzi wangu
nasema hivi…nitamuua kwa mikono yangu mwenyewe.Haina haja ya kuishi
wakati hana sifa ya kumfanya hai. Eti mume, mume gani bwege kilasiku
hapandi kitandani mpaka nishikwe na usingizi ndio nae apande!!!!”
“Hatakama ingelikuwa mimi.Ningetumia akili hiyo hiyo.Unafikiri ni kazi ndogo hiyo…fedheha bwana!”
Mzee
Jophu na Getruda alikunjwa na kuondoka zao.Walielekea nyumba moja ya
wageni ambako waliingiza gari la Gertuda na kujipumzisha.
**************
Katika maisha yangu nina kijitabia fulani cha kutotoka siku za mwisho wa wiki,isipokuwa jioni
tena nikiwa na mke wangu ,Getruda. Huwa natoka katika matembezi mafupi
na kurudi nyumbani.Juma pili hii ilikuwa ngumu kwangu.Kwanza mke wangu
hakuwepo,usishangae nikimuita mke wangu japo sikufanikiwa kufanya tendo
la ndoa.Ni mke wangu kwa sababu nimefunga ndoa kanisani.
Mawazo
bado yalinizonga sana akilini,niliwaza safari ya ghafla ya mke
wangu.Nilitamani sana nijue maendeleo ya wazazi wake huko mkuu
Rombo.Kingine ni tatizo linaloniletea utata ndani ya ndoa yangu.Nilizidi
kuwaza ,kwanini ugonjwa huo uwe kwangu tu.Kwanini usiwe kwa
fulani?.Nilitamani kunywa bia lakini lakini nikaona si kutatua tatizo
zaidi ya kuliongeza.
Nikiwa
kwenye dimbi la mawazo,nilisikia simu ikiita,nilishituka sana.Kwa
haraka nikaiendea simu ambayo niliiacha Varandani juu ya meza.Nilifikiri
mambo mengi ,nikahisi aliyepiga simu alikuwa mke wangu akinipa habari
za mama yake,nilitegemea kupata habari mbaya kutokana na maneno
aliyoniacha nayo Getruda jana alipokurupuka akionekana wazi kuchanganywa
na hali ya mama yake.Nilipofika nikaiokota simu upesi na kuipokea ,
“Hallo mume wangu.Umzima ?”
“Ndio.Vipi kuhusu hali ya mama.Anaendeleaje?”Nilimwuliza.
“Kidogo amepata ahueni.Kuna uvimbe gotini unamsumbua”
“Utakuja lini?”
“Aaa kesho jioni.Namsaidia kumuuguza hospitalini”
“Sawa.Nimebaki mwenyewe kama mkiwa”
“Usijali mpenzi.Upo nyumbani, na hutoki leo?”
“Ndio,nipo sitoki bila wewe.Kwanza najisikia vibaya kabisa sijui ni kwanini mpenzi”
“Pole sana mume wangu,bye”
Getruda akakata simu.
*********************
Kulikuwa na kundi la patao watu watano,aliyekuwa
msemaji mkuu akiwa mzee Jophu.Pembeni aliketi Getruda na kushoto kwake
mwanaume mmoja mwanye umbo kubwa,unaweza ukamfananisha na mcheza
mweleka.Mikono yake minene iliyojaa na kujengeka misuli.Kushoto kwa
mwanaume yule alikuwepo kijana mwingine,mrefu mwembamba lakini anasura
ya kukatili.Ukimuona lazima ungemtambua kama ni muuaji.Huyu aliweka
bastola kibindoni,bastola aina ya Revolver.Aliyebaki alionekana mdogo
sana,ukitadhimini umri wake ni miaka kumi na tano,alionekana alikulia
mitaani.Huyu ni kibaka mzoefu ,achilia mbali bangi ,sigara na dawa za
kulevya, kuvuta petroli na gundi ya viatu kwake si tatizo.Mtoto huyu
walimtumia sana katika matukio ya ujambazi na upelelezi wa wapi kuna
pesa ,wapi tukaibe leo.
Walicheka
muda mfupi tu baada ya Getruda kukata simu, “Anasemaje huyo maiti”Mzee
Jophu aliuliza akiwa anamtizama Getruda kwa udadisi.
“Anasema leo yupo nyumbani hatoki,ni jambo ambalo liko wazi bila mimi habandui mguu wake.Hivyo kazi yake imeisha”
“Patamu
sana hapo.Naomba vijana wangu waingie kazini.Kama nilivyo waelekeza na
mfanye kwa tahadhari sana msije kubainika kama ninyi ndio
mlioua.Mmenisikia?”
“Mzee usitufundishe hii ndio kazi yetu kama kazi nyingine.Tumeua sana na tutaendelea kuua.Pesa ya
kazi mbele”Alisema jambazi mmoja nene lenye kifua kama
pipa,lilitambulika kwa jina moja tu ‘Man Kaugo’Man Kaugo ana kasumba
moja hataki kufundisha kazi ya uuaji,nasema anaielewa vema na ujuzi huo kwake ume komaa.
“Naona mchukue lita arobaini za petroli.Mzungushie nyumba yake yote na muitie kiberiti”
“Eeee!kuna vitu vyangu vya muhimu.Kwanini msimuue bilakuchoma nyumba”
“Vitu vyako nitakulipa.Tatizo ni nini?”
“Nyumba yamgu.Nilitaka mumuue nibaki na nyumba”
“Nyumba nitakununulia njiro”
“Haya, usinidanganye mpenzi”
“Sikudanganyi.Mimi na wewe kwani wa tani?”
“Hapana”
“Sasa kumbe…” akatulia kidogo kisha akasema, “Nafikiri tumemaliza makomando wangu”
“Pesa zetu bado.”
“Kiasi gani ?”
“Milioni tatu kwa kichwa kimoja”
“Ok,subirini kidogo nakuja.”
Mzee
jophu alitia gari moto na kuondoka zake.alielekea benki ambako
alichukua milioni tano na kuzihifadhi.Hakuchelewa alirudi. “Kamata
milioni tatu hizi.Naomba mharakishe tafadhali”
“Sawa mzee.Utasikia mwenyewe mambo yakijibu”Wale vijana waliondoka zao.
Nilisikia
kama watu wakiongea nje ya jengo langu,kila nilipojaribu kutega sikio
kwa makini,nilishindwa kun’gamua mazungumzo yao.Nilitunguza redio kabisa
,japo nilikuwa macho lakini nilihisi bado kiko usingizini,watu hao
walinikaribia dirishani ,kwambali nikasikia mmoja wapo akisema “Hili
ndilo dirisha lake”
Mwingine
akasema “Basi hapa tumwage petroli nyingi iliafe haraka”kilikuwa
kitendo cha haraka nilisikia petroli ikimwagwa dirishani,nilikurupuka na
kushituka ,nilipofungua macho kumbe nilikuwa nikiota njozi mabaya
kabisa.Kukurupuka kwangu hata mke wangu Suzan ambaye tulibahatika kupata
mtoto wa kiume aitwaye Samji ,alinisikia nikipiga kelele, “Nakufaaaaa”
“Nini
mume wangu?”Suzan, mke wangu aliniuliza akiwa na masalio ya
usingizi.Nilihisi mapigo ya moyo yakinienda mbio utadhani nilikimbia umbali mrefu bila kupumzika.
“Baba samji,ni nini mbona umepiga kelele kiasi hicho?”
“Ndoa yangu inanitesa”Niliropoka nikipikicha macho, sikuamini yale niliyoyaona nikiwa usingizini.
“Ndoa yako inakutesa kivipi?”
“Nafikiri nilikuwa nikiota ndoto ya mateso kabisa”
“Ndoto?.Nilikusikia
hata wakati mwingine ukilia ukiwa usingizini.Nilikutingisha lakini huku
shituika, ulikuwa ukisema Getruda Getruda .Getruda ninani?”Nilitulia
kidogo nikajaribu kumkumbuka, “Getruda ni huyo mwanamke niliyemuoa,
akawa ananitesa”
“Usinidanganye mume wangu.Madhambi unayofanya na mahawara wako ,ndio unayaota usiku?”
“Basi
nisamehe mke wangu,ni ndoto tu.Sina mtu nimpendaye zaidi yako.Sijui
njozi ya ajabu namna hii imetokea wapi.Yote niliyoota hakuna hata kimoja
kilichowahi kunitokea”
Ilikuwa usiku ,majira ya saa kumi na moja.Suzan, mke wangu alinisamehe na tukaanza kusali.
MWISHO
No comments:
Post a Comment