Ni siku nyingine ya jumatatu siku yenye ubize mwingi na pilikapilika za hapa na pale. Binafsi jana jumapili na hata jumamosi sikufanya kabisa kazi yoyote na leo nikasema niamke mapema niweze kuwajibu wale waliokuwa wameniachia maswali na mambo mengine kwenye WhatsApp, kweli nimeamka saa kumi usiku nimekaa kwenye computer nikiwajibu watu hadi saa kumi jioni lakini bado sijaweza kuwamaliza!
Basi nikaona isipite jumatatu bila kukuandikia lolote japo dogo.
Leo nakuletea mbinu rahisi kabisa ya kung’arisha meno yako na yakaonekana meupe na yenye kupendeza.
Namna rahisi ya kung’arisha meno yako
Unahitaji vitu viwili, limau na baking soda au wengine huiita bicardonate of soda nayo ni ile wamama huitumia wanapopika maandazi au mikate, inapatikana maduka ya kawaida hata kwa mangi hapo nje ipo.
Namna ya kuandaa:
- Chukua limau kubwa moja ikate katikati, chuja kupata maji maji yake (juisi) kisha changanya baking soda ya unga kijiko kidogo kimoja cha chai. Changanya vizuri mchanganyiko huo.
- Sukutua kinywa chako vizuri ukitumia mswaki na huo mchanganyiko ndiyo iwe dawa yako ya meno. Sukutua (piga mswaki) taratibu kama dakika 3 hadi 5 hivi na mwisho jisafishe kinywa na maji safi.
Mhimu: Fanya zoezi hili nyakati za jioni au usiku unapokaribia kwenda kulala na ufanye mara moja tu kwa wiki na si zaidi ya hapo kwani unaweza kuharibu fizi zako kwa dawa hii usipokuwa makini.
Ukifanya hivi mara 2 au 4 yaani mwezi mmoja utaona tayari meno yako yameanza kuwa meupe na yanayong’aa na kupendeza.
Vyakula kadhaa vifuatavyo vinasaidia kung’arisha meno yako navyo ni pamoja na machungwa, stawrberry, mapeazi, maziwa na mtindi, maji ya kunywa, jibini (cheese), broccoli, celery, karoti, tufaa (apple), kitunguu maji, mbegu mbegu (kama korosho, karanga, almonds) nk .
Vyakula au vitu vinavyoharibu rangi ya meno ni pamoja na uvutaji tumbaku/sigara, chokoleti, chai ya rangi, kahawa, soda nyeusi na vinywaji vingine baridi vyenye kaffeina.
Nakutakia kazi njema sana …
No comments:
Post a Comment