Sababu inayotufanya kulala vibaya ni kulala karibu ya mwingine.
Wanasayansi wamethibitisha kuwa mtu anayekoroma zaidi ni mwanaume sio mwanamke. na mara nyingi wanawake wanashindwa kulala kwa sababu ya kelele hizo za kukoroma. Ni asilimia ndogo tu ya wanawake wanaokoroma . kwa nini
Inaonyesha kuwa wanawake hupata shida kupata usingizi kwa sababu ya kuwa na majukumu mengi kwa siku nzima. lakini pia kutokana na hayo wanakuwa na tatizo la kukosa kumbukumbu na umakini.
Uchunguzi ulipofanywa , ilionekana wanawake ni wengi wanaopata matatizo ya kulala vizuri kuliko wanaume. Na katika kumbukumbu na umakini pia asilimia kubwa ni wanawake wanapata tatizo hilo kuliko wanaume kwa sababu ya kutokupata usingizi wa kutosha.
Moja ya sababu kubwa ya wanawake kutokupata usingizi wa kutosha ? ni kwa sababu wenza wao wanakoroma sana usiku. kitu ambacho kinawafanya wakose usingizi. Na mara nyingi wengi huamua kuhama chumba na kulala sebuleni.
Wakati kukoroma inaweza kuwa ni kitu cha kwanza cha kuharibika kwa mahusiano. Sio hivyo. Kuna tukio lipo zuri linaweza kuongelewa na wanandoa jinsi ya kupata usingizi mzuri kila mmoja. ili waweze kulala pamoja kwa ajili ya faida ya mahusiano yao na kuishi kwa furaha ndani ya ndoa yao. Kulala vizuri ni muhimu katika maisha yetu kuliko tunavyoelewa.
Wakati mwenza wako anapokuwa ndio sababu ya kutopata usingizi, mahusiano yatakuwa yanayumba. ni vizuri kama mtakaa na kuongea kuhusu jambo hilo , jinsi ya kuepuka kukoroma.
Kwa upande mwingine , mwanaume anaweza kuwa ana tatizo la kukosa pumzi vizuri, anashindwa kupumua. hapati hewa ya kutosha, ndio maana anakutana na tukio hilo la kukoroma. Na hio inaweza ikamletea huzuni kubwa. hali ambayo ni mbaya kiafya.
Ni vizuri kufanya uchunguzi kwa kila mmoja ili kuweza kupata matibabu ya papo hapo. badala ya kusababisha matatizo makubwa yasiokuwa na dawa ya kuponya.
No comments:
Post a Comment