Huenda umeniambia aina tofauti ya mapenzi, Aina ya mapenzi ambayo Hayapo kabisa Ulimwenguni. Aina ya mapenzi ambayo hutokea mara moja tu katika maisha, Aina ya mapenzi usioweza kusahau.
Umeniambia aina ya mapenzi ambayo ni ya mawasiliano, Aina ya mapenzi ambayo huwezi kupuuza ujumbe au za kuleta maswali yasiyoweza kujibika, Aina ya mapenzi yenye kuleta siku njema na amani.
Umeniambia aina ya mapenzi ambayo yanaweza kujaribu kuelewa tofauti zilizopo, na kutatua matatizo. Aina ya mapenzi ambayo hujui jinsi ya kukatia tamaa.
Umeniambia aina ya mapenzi ambayo yanafanya kazi, Aina ya mapenzi ambayo hujionyesha wazi, aina ya mapenzi ambayo husimama imara, Aina ya mapenzi ambayo hayakuachi uteseke.
Umeniambia aina ya mapenzi ambayo husubiri, Aina ya mapenzi ambayo hukaa wakati mambo yanapoharibika, Aina ya mapenzi ambayo hujaribiwa kwa urahisi, Aina ya mapenzi ambayo hayabadiliki kwa siku moja.
Umeniambia aina ya mapenzi ambyo yana uhakika , Aina ya mapenzi ambayo hayavunji ahadi, Aina ya mapenzi ambayo hayavunji moyo, Aina ya mapenzi ambayo yanafanya Ulimwengu uwe ni mahali pazuri.
Na kamwe toka wakati ule , Sitaweza kupata upendo mwingine kama wa kwako, Sitaweza kupata kama wewe, Sitaweza kupata anayeelewa hivyo.Sitaweza kupata yule anayefahamu jinsi ya kupenda.
Nilifikiri aina hii ya mapenzi ni kila kitu, lakini jinsi ninavyojaribu kumpenda mwingine , ndivyo ninapoelewa kuwa huo upendo ulikuwa ni wewe tu—Ambao hakuna mtu ajuaye upendo kama huo hata kidogo.
Lakini bado natafuta Upendo ambao ulinifungulia macho kwa hilo, Aina ya Upendo Unaoponya. kwa sababu aina hii ya mapenzi mapya ni upofu, Na inanifanya niwe mgonjwa.
Napenda tu kinachotokea kwenye mfumo uliopo, napenda kinachotokea kwenye mwili wangu wakati tukiwa pamoja , Sipati mapenzi ya thamani ya juu ya kutosheka . Hii yote ni kwa sababu sikufahamu kuwa kila mtu ni tofauti, kila mtu ana aina yake ya kupenda, kila mtu ana lugha yake ya mapenzi. Haiwezi kufanana, Hicho ndicho nilitakiwa kujifunza.
No comments:
Post a Comment