Artikel Terbaru

Responsive Ads Here

Thursday, August 24, 2017

Vijana Miaka 20, 25 Fahamuni Ukweli Huu Mdogo




1.Shahada ya Chuo Sio sawa na Mafanikio
2.Kung’ang’ana na marafiki ambao ni sumu  watakusababishia  madhara makubwa mbeleni.
3.Sio dhambi kuwa Single
4.Unaruhusiwa kuwa single na kuwa mwenye furaha
5.Hata hili linapita tu.
6.Sio kila mahusiano yalitakiwa yawe ya kudumu. mengine ni mafunzo kwako.
7.Kubali makosa unayofanya katika maisha yako.
8.Umri wako ni mgumu kukabiliana  na mambo  wakati mwingine. keep going.
9.Using’ang’ane na Kazi moja tu.
10.Achana na watu wanaokuangusha katika maisha.
11.Jifunze kuachana na mtu kwa njia sahihi. Usitukane mtu kwa sababu yoyote. wala kutuma ujumbe mbaya.
12.Usidharau moyo wako
13.Siku zote uwe na akili nzuri na usiombe msamaha kwa hilo
14.Fahamu kwamba uponyaji sio kitu cha rahisi.
15.Bila siku mbaya usingeweza kuwa na siku nzuri.
16.Karibu kila mtu hujisikia kuwa yuko nyuma sio wewe tu.
17.Acha kujali hizo like za kwenye facebook, intagram. mwisho hutaweza kujipenda mwenyewe. 
18.Mwonekano wako sio tija,  kitu kizuri ni jinsi gani unawapenda watu na kuwafanyia vizuri.
19.Shikilia marafiki wazuri ulionao.
20.Wewe ni mtu pekee Ulimwenguni. Sambaza mwanga wako
21.Jifunze jinsi ya kumsikiliza mtu anayelalamika
22.Pumzika na upumue kwa muda
23.Wakati mwingine kutembea itakupa afya nzuri  ya akili.
24.Kama upo katika kutafuta, Usijiingize kwenye woga na kujiona kama mzigo.
25.Sikiliza zaidi
26.Hata kama maneno yako  hayasikilizwi. Upo wakati utakuja kusikilizwa katika maisha yako.
27.Yapo mambo mengi katika maisha  zaidi ya kuoa au kuolewa.
28.Ni kupoteza muda ukiwa unaona wivu kwa wengine.
29.Kitu pekee cha kufanya ni kuwa mtu wa kujitolea katika maisha yako.
30.Wakumbatie wazazi wako zaidi kwa sababu ipo siku hutaweza kufanya hivyo.
31.Kama hujui ni vipi au kwa nini unahisi kwa namna hio , badilisha kuwa sanaa.
32.Kila pumzi unayovuta na kutoa ni zawadi
33.Tiba ni njia bora ya kujifunza zaidi kuhusu wewe na  kujiweka vizuri kwa wakati mmoja.
34.Marafiki wazuri ni ngumu kuwapata. Usiwadharau 
35.Wakati mwingine unahitaji tu kulia . Usione aibu kwa ajili hio.
36.Achilia kisichokuwa cha kwako.  kumshikilia mtu au kazi ambayo sio nzuri kwako, utajikuta pabaya.
37.Kila mtu anapambana. Sio peke yako.
38.Siku moja utakuja kuona hayo matatizo kuwa ni mwalimu wako mzuri na utafurahia kwa sababu yalitokea.
39.Jitahidi kufanya Meditation japo dakika 10 kila siku. Hutajilaumu.
40 Zaidi ya yote, jifunze kujipenda mwenywe, kujijali, kujiheshimu, kujitambua na kujikubali wewe mwenyewe. Jifanyie wema mwenyewe. Mungu awe ni kipaumbele chako.

No comments:

Post a Comment