Upendo usio na masharti Hautokei tu vyovyote. Mwanzoni mwa mahusiano ya kimapenzi, upendo wa juu unaokuja kwako na kukufanya ujisikie kumpenda mtu. Upendo huo ni Upendo wa tofauti.
Upendo mpya mara zote hauna masharti
Kitu cha kwanza kinachovuta umakini wako ni kitu kinachofanana. Macho yao mazuri, kucheka kwao. Mnapoanza kufahamiana wote wawili, utaona kwamba mnapenda aina moja ya music, aina moja ya chakula. humchoki huyu mtu na kuona kama mtadumu kwa pamoja.
Mambo kama haya yanakufanya ujione kama uko kwenye mapenzi . Lakini sio Upendo ambao hauna masharti, upendo ambao hauna sababu; ni Kupendezewa tu. Ukweli ni kwamba upendo huu unaingizwa uongo wenye tabia za juu. Mahusiano yanapoendelea kukua, upendo huo unapungua, Yale mapenzi uliozoea kuyaona yanakwisha. hutaona kucheka kwao tena . hutaona macho mazuri tena.
Jiulize ni aina gani ya Upendo Ulinao Wa kawaida
Thamani yako inaonekana katika hatua hii ya mahusiano. Mwenza wako anajisikiaje kuhusu yeye mwenyewe, Kisiasa, mambo ya kijamii yana umuhimu gani kwake. Kwa sababu kama hamtaweza kushirikishana thamani zenu za ndani, utatambua kwamba mpo hapo pamoja kwa sababu ya uzuri wa mtu wa uso na kucheka kwake na vitu vyake .
Katika hatua hii ya mahusiano. utaanza kupima na kuchambua upendo huo mlionao. unaweza kuwa hata na hofu au mashaka, Utajiuliza mwenyewe, Huu ni upendo wa kweli au upendo wa sababu fulani? kitu wanachokitaka katika hatua hii ni kuwa na uhakika kama wapo kwenye upendo wa kweli ili kudumisha mahusiano yao na kufanya maamuzi makubwa ya maisha. Kama walikuwa bado kuoana , wataamua kuoana.
Kuolewa na kupata mtoto ni maamuzi yanayofanywa baada ya kuona msimamo wa mtu uko wapi. Wengine wanaangalia uwezo wa mtu mmoja. hasa wanaweka walio wengi huangalia kipato cha mtu cha kutunza familia. Kitu ambacho ni kweli.
Ni kawaida kabisa kuanza kujiuliza aina gani ya upendo unaoingia. Hii ni muhimu kwa sababu mnataka kuishi pamoja . Na ukifikia hatua hii unahitaji kujua upendo usio na sababu ni upi?
Upendo ambao hauna sababu au mashati sio, ”Haijalishi unafanya nini”
Watu wengi wanafikiri kwamba upendo huu una maana kuwa unakaa na mtu haijalishi kitu gani anachokifanya. Wanafikiri kwamba upendo wa kweli ni kuishi tu na mtu bila ya kujali kitu na bila ya kukata tamaa. Hali hii ni ya hatari sana, inapelekea watu wengi kubaki katika mahusiano ya kunyanyasika. Mambo ambayo mwenza wako anafanya kila siku yanakuathiri maisha yako, hisia zako, uhai wako. unatakiwa kuangalia kwa makini matendo yao.
Upendo usio na sababu ni huu. utampenda mwenza wako haijalishi kitu gani kimemtokea. Kama mwenza wako kapatwa na tatizo baya kama ugonjwa, upendo usio na masharti una maana kwamba utabaki naye , utakuwepo upande wake kwa kila kitu wakati anapokuwa kwenye matibabu. kama amepata ajali mbaya, au kama amapoteza kazi yake , utakuwepo pale naye. hali hii ya kujitoa kwa aina hii ndio upendo usio na masharti.
Upande wa mwenza aliyepata matatizo naye , asichukulie kama ni faida anapokuwa anapewa upendo huo. Naye inabidi aonyeshe umuhimu wa mwenza wake kwa kuwepo pale kuwa ni zawadi kubwa.
Lakini ndani ya upendo huu upo wakati utaonyesha kutopendezwa na kitu fulani, na hio ni kawaida kabisa. huwezi kupenda kila kitu. Kupenda kila kitu ina maana kwamba unaangalia tabia nzuri peke yake. Hakuna mtu mkamilifu , kila mtu ana madhaifu, kila mtu anafanya makosa.
Upendo usio na sababu sio ule wa kutaka kumlinda mwenza wako.
Ngoja tuweke kitu wazi hapa. Hakuna mtu anayependa kuona kitu kibaya kinampata mtu anayempenda. hamu ya kumlinda mwenza wako ni jukumu la kawaida kwenye mahusiano yenu. Wakati mwingine, ingawa kuweka ulinzi zaidi ipo katika mpangilio uliopo.
Unapokuwa na upendo huo kwa mwenza wako, utapenda kuona malengo yao yanafanikiwa. Ingawa katika hatua hii yapo maumivu. lakini kama unampenda kweli utamuelewa na hutaepuka ila utamsaidia kufika mahali alipokuwa anataka kufika.
Upendo huu wa kweli utawaruhusu kupata mabadiliko ya pamoja.
Mtasaidiana, mtakua pamoja, mtashirikishana thamani zenu, hamtabadilika, mtakuwa wenye furaha, mnakuwa huru kila mtu. kila mtu atatimiza malengo yake. mtaelewana, Mtasameheana. kila mtu atamshukuru mwenzake .
Kujifahamu na kujipenda, kujijali mwenyewe, itakusaidia kumpenda mwenza wako bila ya masharti.
No comments:
Post a Comment