Ok najua ushawahi kuona jambo kama hili katika sinema si mara moja wala mara mbili...
Majambazi waliobanywa ambao wamevamia benki wakiwa ndani na bunduki zao huku wakitishia kuua mateka wao...
Ama jamaa ambaye amekumbwa na misongo ya mawazo (stress) amesimama
katika ncha ya ukuta wa jumba lenye ghorofa 30 na anatishia kujirusha...
Hatua aina hii utapata polisi wakimuita mtu mahususi aka mpatanishi
ambaye atahitajika kuongea na watu aina hii kwa amani bila kutokea jambo
lolote baya...
Watu hawa huwa wamefundishwa spesheli kutatua aina hii ya migogoro na
hakuna anayeweza kuwashinda kwa ujuzi wao dunia hii. Wanajua jinsi ya
kutumia maneno na lugha MAHUSUSI ambayo itamfanya mtu kusisimka kihisia
na kuweza kuwakontrol vile ambavyo wanataka wao.
Wanayajua maneno ambayo yanafanya kazi kama hirizi ambayo yatamfanya mtu kutulia na kumfanya aamini kila kitu ambacho ataongea.
So, je mbinu hii unaweza kuitumia kwa mwanamke?
Mbinu hii mwanzo ni rahisi sana kuitumia kwa mwanamke. Hii ni kwa sababu
mara ya kwanza unapokutana na mwanamke na kuanza kumuongelesha huwa
hajiskii huru na uwepo wako, huwa kwa kawaida anajiskia kama wewe uko
hapo na unamtatiza shughli yake ambayo alikuwa akifanya. So kitu cha
kwanza cha kufanya huwa unajaribu kumuonyesha kuwa wewe ni mtu salama na
unaomba muda wake kiasi uongee naye (inajirudia katika hali ya mtekaji
nyara na mpatanishi)
Zama nami...
Ok mwanzo nafaa nianze kwa kueleza hivi kwa wale ambao hawajajua mbinu hii.
Kuna kitu ambacho huwa kinatokea katika situation ya utekaji nyara:
Watekaji nyara kwa kawaida huwa na hofu mwingi muda wote. Kwa kawaida
hukumbwa na misongo ya mawazo muda wote ambao watakuwa na mateka wao.
Hii ni kama vile mwanamke anapopandwa na misongo ya mawazo asiyoweza
kuizuia wakati wowote ambao mwanaume asiyemjua anamuapproach na kuanza
kumtongoza.
So katika hali kama hii, unapaswa kujua jinsi ya KUONDOA misongo yake ya
mawazo na UJENGE MSHIKAMANO na yeye haraka iwezekanavyo.
Unapaswa kutumia maneno yafaayo ambayo yatamfanya apumzike na kutulia...
Na kufanikisha haya yote hupaswi kutumia maneno ambayo yanachosha kama vile...
"Hivi wewe waitwa nani?"
"Ushawahi kuwa hapa awali?"
"Unafanya kazi gani?"
....na maneno mengine aina hii ambayo yanachosha.
Hapa lazima utumie maneno ambayo yatakuwa kama kitufe ambacho ukikifinya
tu atakufungukia na kukuambia kila kitu ambacho unataka aseme...
Na unayavuta maongezi yenu mbali na 'sehemu hatari' ambazo zinaweza
kusababisha yeye kupoteza hamu na wewe (90% ya wanaume hufanya MAKOSA
HAYA ya kuleta mada ambazo zinawaudhi wanawake...)
Na wakati uo huo, unaingiza mbinu na maujanja rahisi ambayo yatachangamsha hisia chanya na kuondoa ukinzani wowote...
Kwa lugha nyepesi namaanisha ya kuwa lazima ujue jinsi ya kucontrol
Zifuatazo ni baadhi ya hali na jinsi ya kuzitatua...
Hali: Unataka kumtoa out mwanamke lakini hujui ni vipi atareact.
Mbinu: Watekaji nyara huwa wanapenda kuhakikishiwa usalama wao
iwapo watajisalimisha kwa amani. Hivyo mpatanishi huelezea kabisa yale
yote ambayo yatakayojiri baada ya kujisalimisa ili kuondoa woga wowote.
Atasema hivi: Nataka tu ujue Papito, kama utajitokeza na kuongea na
mimi, hakuna mtu atakutatiza. Ni mimi na wewe tu ambao
tutaongea...hakuna cha zaidi.
Vivyo hivyo kwa mwanamke, unafaa kumwambia yatakayojiri. Bila hivyo
atakuwa akijiuliza ni KITU GANI ambacho kitakachotokea akikubali
mwitikio wako wa kutoka out na wewe.
(Je unajaribu kuingia katika chupi yake? Ama wataka kumpeleka katika
sehemu ambayo itamboa na ambayo haitamstarehesha? Ni kitu gani ambacho
kitatokea kati yako na yeye??)
Mwambie hivi: "Nataka kukupeleka katika huu mkahawa/klabu ambayo
niliivumbua hivi karibuni... ni sehemu nzuri ambayo naamini utaipenda
kwa sababu wanacheza nyimbo nzuri na za kuvutia, mwanzo sehemu hii
inalingana na ladha yako. Ntakuwa huko usiku wa Ijumaa, mbona tusiende
pamoja na wewe wakati wa saa tatu usiku? Huwa sipendi kuchelewa sana
nikiwa nje usiku lakini nikiwa na wewe nitaspend muda mrefu kiasi na
wewe ili tujiinjoy zaidi...."
Hapa utakuwa ushaeleza matokeo yote yatakayojiri akiwa na wewe usiku huo.
(Kwa kutumia mbinu hii, utakuwa ushamjulisha matokeo yote ambayo
yatatokea USIKU HUO kimukhtasari, lakini utakuwa umeweka plan yako kwa
njia ambayo inaonekana ni nzuri na ambayo haimtishii. Utakuwa
umerahisisha kwake kukubali na kusema "ndio")
******
Hali: Anaendelea kuzidi kukutajia kuhusu ex boyfriend wake, na kila wakati akimtaja anaharibu hisia za mazungumzo.
Mbinu: Mfanye ex boyfriend wake asionekane na thamani yeyote na
'kuziondoa nguvu zake zote' kwa kumrejelea kama "yule
mwanaume"...halafu unajeuza mada mliokuwa mkiongea.
Mfano...
Wewe: "Unajua Mamito, inaonekana kama YULE MWANAUME kiukweli
hakuwa katika level yako hivyo ilikuwa jambo zuri kuachana naye. Nahisi
kuna mengine muhimu zaidi ambayo yanakufaa kumliko...hebu niambie zaidi
kuhusu kazi yako, naona inavutia zaidi kuona kuwa wewe ni (TAJA KAZI
ANAYOFANYA)"
Wapatanishi hutumia mbinu ii hii wakati wanapotaja 'bunduki' ama
'bomu'...hakuna wakati watasema "Nataka uishushe bunduki yako," hii ni
kwa sababu hilo NENO MOJA litamsisimua mtekaji nyara na kuongeza levels
zake za stress.
Badala yake, wao husema "Ni mimi na wewe pekee tunaoongea, Papito, so nataka utulie na uweke HICHO KITU chini..."
(Na kufanya hivi wanaanza kuongea kuhusu maswala mengine ambayo yanajenga mshikamano wa nguvu...)
Psss...soma (sehemu ya pili ya chapisho hili)
Monday, April 30, 2018
Jinsi Ya Kuwasiliana Na Wanawake Na Mbinu Ya 'Wapatanishi Mateka'
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment