k. Inaweza kuonekana jambo la kufurahisha, lakini katika Nesi Mapenzi,
tunaona ya kuwa ufuoni mwa bahari ni sehemu moja nzuri zaidi ya kukutana
na wanawake wapya. Kama unaishi karibu na ufuo wa bahari halafu
hujajishughulisha kutafuta mchumba huko basi ni wakati wako wa kufikiria
mara ya pili: Tumia muda wako vizuri kwa kumakinika na kuapproach
wanawake sehemu hizo na utakuja kugundua kwa nini tunasema kuwa beach ni
sehemu moja muhimu ya kuapproach wanawake.
Na kwa kusistiza msimamo wetu, tumekuja na sababu zifuatazo:
1. Kunafurahisha
Hakuna njia mbili kuhusiana na swala hili: Ufuo wa bahari huwa ni sehemu
inayofurahisha. So wakati ambapo unaanza kuongea na mwanamke katika
ufuo wa bahari, nafasi kuu zaidi ni kuwa tayari anaenjoy muda wake
katika sehemu hio. Hii inamaanisha hakutakuwa na haja za kuziondoa hisia
zozote hasi. Atakuwa anafuraha, mcheshi, anajienjoy, na pia
itakuwa rahisi kwake kukusikiliza kwa urahisi kwa sababu muda wote
amejawa na furaha. Katika ufuo wa bahari ni rahisi sana ukilinganisha na
maktabani, gym ama hata katika mkahawa. So tumia hii nafasi
inayojitokeza.
2. Unakuwa mchangamfu
Ok. mtakubaliana nami ya kuwa hakuna mtu atajipeleka kwa ufuo wa bahari
kama hana kitu cha kufanya. Kwa kawaida mtu akienda beach huwa lengo
lake kuu ni kuogelea, hujumuika na marafiki zake, kucheza mpira,
kukimbia ama jambo lolote lile ilimradi tu aonekane yuko mchangamfu na
shughli flani. Kumhusisha mwanamke katika shughli zako ni njia muhimu na
ya kwanza kuchukua ili uweze kumfahamu zaidi. Bora zaidi ni kama
unafanya beach party, unaweza kumualika kwa marafiki zako. Cha zaidi ni
kuwa wakati ambapo unaonekana mchangamfu, pia unaonekana bora, jambo
ambalo ni muhimu.
3. Ni sehemu ambayo wanawake hupenda
Kila mtu anajua ya kuwa sehemu za ufuo wa bahari kuna wanawake wengi
zaidi kuliko sehemu zozote zile ambazo zinajulikana. Kama unataka
kukutana na wanawake basi ni lazima uende katika zile sehemu ambazo
wanapatikana. So bila kupoteza wakati wako unafaa utembelee sehemu hizi
haswa beach ambayo uko karibu nayo uweze kutangamana na wanawake tofauti
tofauti.
Halafu alama muhimu hapa ni kuwa katika beach kwa kawaida wanawake huwa
wamevalia bikini na vinguo vya kuogelea. So kama unatafuta sehemu ya
kutafuta wanawake, hata si jambo la kutumia ubongo. Hivyo basi mbona
hujaenda kwa beach tayari?
4. Hisia zako zinakuwa juu
Uko mchangamfu, unaangazwa na jua la ufuoni na unajienjoy. Kuna nafasi
gani nyingine unangojea upewe ili uongee na wanawake? Sehemu kama hii
unapaswa uonyeshe hisia za juu, ujihisi bingwa na kufurahia wakati
unapoongea na wanawake. Kama wewe ni mwanaume ambaye unapenda beach
halafu unapenda maji, hakuna njia mbili za kuchagua, lazima uende
baharini na uanze kukutana na wanawake wapya, sehemu ambayo itainua
hisia zako.
5. Ni romantic
Labda maswala ya romantiki huna lakini yeye akawa nayo. Huu hapa ni uzuri wa romantic ambazo
zinajikuza kutokana na mapenzi ya baharini: ni kuwa neno 'Nimefurahi
kukutana na wewe" litajeuka kuwa "nataka kukujua zaidi" hadi likawa
"nakumbuka ule wakati tulipokutana mara ya kwanza...".
Hakuna sehemu nyingine yeyote ile ambayo unaweza kuwa na nafasi ya
kuupiga jeki uhusiano wako na mwanamke ambaye umekutana naye kidharura
isipokuwa katika ufuo wa bahari. [Soma: Siri za kumvutia mwanamke]
Monday, April 30, 2018
Sababu 5 Za Kutongoza Wanawake Ufuoni Mwa Bahari
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment