1. Ugonjwa wa kaswende.
Kitaalamu
kama syphilis, huu ni ugonjwa hatari sana ambao umeharibu maisha ya
watu wengi bila wao kujifahamu. Ugonjwa huu ambao huambukizwa kwa njia
ya kujamiana huanza kidogo na kidonda ambacho hakiumi sehemu ambapo
wadudu wamepita mfano mdomoni au sehemu za siri.
Kidonda
hicho hupona, upele usiowasha hutokea na baadae vyote hivyo hupotea.
Ugonjwa huu baadae huingia ndani ya mwili na kuuanza kuharibu viungo vya
ndani. Mwisho kabisa ugonjwa huu huahamia kwenye ubongo na kumfanya mtu
kua kichaa.
2. Ugonjwa wa hepatitis B.
Ugonjwa
huu ni hatari na unaua haraka kuliko ukimwi, virusi vya ugonjwa huu
huambukizwa kwa njia ya kujamiana na kugusana kwa damu au majimaji ya
mwili kama ukimwi lakini ni rahisi zaidi kuambukizwa ugonjwa huu kuliko
kupata ukimwi.
Ugonjwa
huu hushambulia maini na kuacha makovu, Mgonjwa hupata macho ya njano,
homa, maumivu ya kichwa na kadhalika. Ugonjwa hii mwishoni hupelekea
kansa ya ini ambayo inaua ndani ya miezi sita.
3. Ugonjwa wa ukimwi.
Huu ni ugonjwa unaofahamika kwani unatangazwa sana hasa kwenye vituo vya Radio, Tv, Magazeti na sehemu mbalimbali.
Ugonjwa
huu uligundulika karne ya 20 na mpaka sasa umeshaua watu wengi sana na
zaidi ya 95% ya wagonjwa waliambukizwa kwa kushiriki ngono bila kinga.
4. Ugonjwa wa gonorea.
Huu
ni ugonjwa wa zinaa ambao unashambulia jinsia zote yaani Wanaume na
Wanawake, mara nyingi Mwanaume hawezi kujificha na ugonjwa huu kwani
dalili za ugonjwa huo kama kutoka na usaa kwenye njia ya kukojolea
zitamuumbua lakini kwa wananwake ugonjwa huu huweza kukaa kimya na mwana
mke hujikuta akisambaza ugonjwa huo bila kujua. Mwishoni ugonjwa huu
hushambulia kizazi na kusababisha ugumba.
Saturday, April 7, 2018
Kabla ya kufunga ndoa hakikisha mmepima haya magonjwa 4 ya kuambukizwa
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment