Kama inavyotambulika ni kuwa ni rahisi sana kutumia jumbe fupi
kuwasiliana na mwingine kupitisha ujumbe. Lakini je huo ujumbe unaoutuma
unachukuliwa vipi na unayemtumia?
Katika swala la kutongoza ama kumSMS mwanamke, wanaume wengine wanafanya
makosa makubwa wakati wanapochat bila wao kujua. Jambo ambalo nimeamua
kuliweka wazi.
(Kwa bahati mbaya ni kuwa makosa haya yanafanywa na wanaume kila wakati)
1. SMS za kujisifu
Kosa hili nishawahi kulizungumzia mara kwa mara kwa blog hii, na ni
wanaume wengi sana wanapenda kulifanya. Najua waelewa nazungumza kuhusu
nini. Kuongea stori za kirare (na 85% ya ufala) ambazo unajaribu
kumwonyesha mwanamke jinsi ulivyo burudi, kumwonyesha kuwa una marafiki
wazuri ambao wanaweza kukufanyia chochote kile utakacho, na kuwa huwa
unatembea sehemu tofauti tofauti za kifahari kwa kuwa umefanikiwa na una
umuhimu mkubwa katika jamii.
Kwa maneno ya urahisi ni kuwa unajaribu kadri iwezekanavyo kumpendeza mwanamke.
Mwanamke wako mwenye hadhi atayaringa macho yake na kucheka kimoyo
akianza kuhisi kama unafanya hivyo kumpendeza. Kwa nini? Kwa sababu
unajaribu kutumia mbinu hio kumfanya akupende. Ni wakati wako wa kuacha
kutumia mwanamke meseji kama hizi.
2. Kuwa na mapepe
Kumualika mtoke deti pamoja kabla ya kutumia mbinu ya kumtongoza ili
akukubali. Hakuna njia nyingine nzuri zaidi ya hii kudhihirisha kuwa
wewe:
(a) una experience ndogo ya kutangamana na kuwajua wanawake (b) hauna ladha ya maana kuchagua wanawake
(PssS: Kama kujuana kwenu kulikuwa kwa nishati, unaweza kuipuuza hii)
3. Kupumbazika kwake
Unamtumia mamia ya text za ucheshi, unamsuka, unamwelezea stori za ovyo
ovyo za abunuwasi na nyingine, na unazidi kumtumia sms za 'kumvutia'
zaidi --mpaka inafikia mahali flani unamboa na anaanza kukupuuza.
So imekuwaje mpaka ameanza kukupuuza? Umempandisha mzuka wa kukupenda halafu ukapoesha kila kitu.
Wanawake wanadhania ya kuwa mwanaume ambaye anaonyesha interest kwao
halafu hataki watoke deti pamoja huwa ni mwoga wa kuchukua hatua ya
mbele.
4. Kuharibu tenshen
Unafafanua jokes zako kuhakikishia ya kuwa anaelewa kile unachomaanisha.
Unajihisi haujiskii vizuri kama hujibu texts zake, kwa sababu hutaki
aone kama unampuuza. Kama anakataa na kitu flani, unanyenyekea na
kukubaliana na kila atakachosema.
Hii inaonyesha ya kuwa wewe si mwanaume dhabiti, kwa sababu hauwezi kuhimili tenshen, na mbaya zaidi ni kuwa unaogopa kumpoteza.
5. Mambo yakienda mrama
Wakati ambapo amekataa ama kusimama kureply text zako, unaanza kutoa kucha zako za ujinga na ''kumweka sehemu anayostahili''
Unaanza kumwambia jinsi alivyo mbovu, anatisha, ni zuzu ama mpotezea
watu wakati, ama ni mwanamke mwenye hadhi ya chini na unaweza kufanya
zaidi. (Kwa mwanamke atakuwa akifikiria, ''Ha ha, haukuwa unasema hivyo
dakika mbili zilizopita ulipodhania una nafasi kwangu'')
Okay...
Najua kuwa text zako ni za level ya juu wakati unapomtext mwanamke, na
naamini hauwezi kufanya makosa tuliyoyaeleza hapo juu. Lakini tukiwa
waadilifu ni kuwa tunaweza kukubali kufanya kosa moja au lingine katika
haya.

No comments:
Post a Comment