ONYO: kuna baadhi ya watu ambao wanaweza kuona machapisho aina hii kukosa maadili kijamii. Kama utaona kuwa utazilika ama kuudhika na post hizi, tafadhali itakuwa vyema kama hautaendelea kusoma zaidi ya hapa.
So katika msururu wetu wa machaposho aina hii tumeanza na:
Jinsi ya kumshawishi mwanamke kutoka kwa mwanaume mwingine
Katika post ya mbeleni tulieleze kwa upana jinsi ya kumtongoza na
kumshawishi mwanamke ambaye ana boyfriend, leo tumeamua kuingia kwa
undani zaidi kwa kutumia sanaa ya mazungumzo kwa kutumia mbinu ya kiini
macho kumfanya amchukie boyfriend wake.
Kabla kutumia mbinu hii, lazima mwanaume ajenge uhusiano mwema baina
yake na mwanamke. Kuwa na uhusiano mwema baina yako na mwanamke kutakupa
wewe uwezo wa urahisi kufanya kile ambacho unataka kwa mwanamke yeyote.
Ok. Tukirudi kwa sanaa hii, kile ambacho unafaa kufanya ni kutumia
maswali ambayo yamepakizwa tayari na ambayo yatamfanya yeye kujipima
thamani yake.... halafu utamlazimisha kugundua ila zote za mpenzi
wake/boyfriend. Ni fioa, siri, na mbinu ya kuzimu.
Hili ndilo swali la ulozi ambalo unafaa kuanza kumuuliza:
'Unajua nini, nimekuwa na shauku kutaka kujua ni sababu gani mwanamke
anashikika sana kwa mpenzi wake. Ni kitu gani cha kwanza ambacho
kilikuvutia kwa boyfriend wako?'
Mara ya kwanza ataliona swali hili ni geni kwa nini umetaka kujua zaidi
kumhusu boyfriend wake, lakini kile ambacho unataka ni kumfanya yeye
kuelezea kumhusu boyfriend wake zaidi kadri iwezekanavyo. So unafaa
kuufuata mkondo huu wa maswali-
- "ni kitu gani unachopenda kumhusu?"
- "kiukweli unamhisi vipi hisia zake kwako? (muulize zaidi)
- "katika fikra zako kidunia, ungetamani kuwa na boyfriend kamili mwenye sifa zipi?" (mfanye ayafananishe matamanio yake)
Kile ambacho unafanya hapa ni kumpa nafasi ya kipekee ya kuongea mabaya
kumhusu boyfriend wake. Wakati ambapo ataanza kuingia kueleza mambo hasi
kumhusu boyfriend wake, mhimize aongee zaidi kwa kumuuliza aeleze kwa
kina. Mfano akisema "nachukia tabia ya boyfriend wangu kunikasirikia kwa
sababu ndogo ndogo" wewe unaweza kumuuliza "kukasirika kwa sababu kama
zipi zinazokuudhi?" nk.
Ok. Hii hapa ni mbinu ya maswali ya kumuuliza kumfanya aue hisia zake za
boyfriend wake asilani -tumia saikolojia mjeuko kumfanya akudhihirishie
kuwa boyfriend wake ni mbaya.
-"bila shaka hakugundua kama alikuwa akifanya..."
-"lakini anaonekana si mbaya sana..."
-"labda amekuwa akifanya hivyo kwa sababu wa mapenzi yenu..."
Ujanja hapa ni kuwa MSIRI iwezekanavyo, na haufai kumfanya agundue ya
kuwa unafanya amfikirie boyfriend wake kama mtu mbaya. Iwapo wewe una
azma ya kuwa mwangamizaji wa mahusiano basi unafaa kufahamu jinsi ya
kutumia mbinu hii ili kumfanya mwanamke akupende bila yeye kuelewa
sababu za kwake kukuzimia.
Kama wataka kujua mbinu hii kwa kina fanya kulike page ya Nesi Mapenzi
na mtoe request nyingi kupitia kwa inbox ili admin wa blog hii aweze
kuidhinisha post inayofafanua zaidi.

No comments:
Post a Comment