Inapita miezi mitatu mkiwa pamoja na huyu mwanaume uliyemzimia, lakini kuna kitu kuhusu mahusiano yenu ambacho kinayafanya mahusiano yenu yasiwe ya shangwe tena. Imepita miezi kadhaa tangu mtoke deti ya kwanza lakini bado hajakufanya wewe kuwa wake. Inafikia pahala flani unaanza kujiuliza iwapo umekuwa ukipoteza muda wako na mwanaume huyu ama bado ni mapema kukata tamaa.
Hili ni jambo la kawaida linalojitokeza kwa wanawake ambao ni single, na ni rahisi sana kuliepuka. Mwanaume ambaye anajitolea kwa mahusiano huwa anaonyesha dalili mwezi wa kwanza wa kudetiana, hivyo lazima uzijue dalili hizi bila kupotezewa wakati wako.
Mwanaume ambaye anajitolea kwa mahusiano utamjua tu, hii ni kwa sababu atafanya juu chini kuhakikisha ya kuwa mahusiano yenu yanakuwa ya shangwe na kuona kuwa una furaha.
Kila siku zinaposonga kwa kudeti na mwanaume, ndipo interest ya kwake inapungua kuwa boyfriend wako kama itapita miezi mitatu bila yeye kuchukua hatua zozote za kuyapanua mahusiano yenu.
So utajuaje kama mwanaume hatakuwa boyfriend wako?
1. Kama unalala na yeye
Hili si jambo geni. Kulingana na wanaume, wao husema ya kuwa hata kama
mwanamke awe mrembo kiasi gani, pindi atakapoanza kulala naye, hupoteza
interest kwake. Wazo hili pia limedhibitishwa na wanasayasi kuwa wanaume
wanapoteza hamu na mwanamke pindi wanapolala naye.
Hivyo kama mwanamke hufai kutumia nafasi hii ya kumridhisha mwanaume kwa
kufanya ngono ukidhania ya kuwa ni silaha yako kuu ya kumnasa. Ngono ni
kihamasisho kwa mwanaume na wala si kitu ambacho ni haki yake.
Ni vizuri zaidi kujizuia kutofanya mapenzi na mwanaume hadi ile siku
atachukua majukumu yake ya kuendeleza mahusiano yenu mbele. Ukichukua
hatua ya kulala na mwanaume mapema utamfanya asijitolee kuendeleza
mahusiano yenu.
2. Kama hakuhusishi na mipango yake
Mwanaume ambaye anataka wewe kuwa boyfriend wake atakuhusisha na maisha
yake. Lakini kama unajua mipango yake na shughli zake mkiwa naye halafu
msipokuwa pamoja hujui mambo yake basi ni dhahiri ya kuwa mwanaume kama
huyu hana maslahi yeyote kwako.
Tatizo ni kuwa wanawake wengine hukataa kuamini jambo hili. Ok
tuchukulie hivi, wewe kama unampenda mtu fulani ungependa kuwajulisha
kitu chochote ambacho unafanya. Hii ni kwa sababu unataka kuwahusisha na
maisha yako ili wamakinike sana na wewe.
Vivyo hivyo, mwanaume ambaye amejitolea kuchukua majukumu ya kuendeleza
mahusiano yenu huwa anagawa mikakati na mambo yake kwako. Huwa anafanya
hivyo ili kuhakikisha ya kuwa hakutakuwa na mwingine ambaye
atakushawishi, atafanya juu chini kuona anafanikiwa kwako.
Hii ni tofauti na mwanaume ambaye atapotea wikendi nzima halafu akupigie
simu siku nyingine. Mwanaume kama huyu hayuko serious na mara nyingi ni
kuwa aina hii ya wanaume lengo lao ni kukuchezea ama huwa na wanawake
wengine wengi.
3. Hakufukuzii
Kuna tofauti kubwa kati ya kukimbiza na kufukuzia. Unaweza kukimbiza
kitu ambacho kinakimbia kutoka kwako. Kama mwanaume ameonyesha interest
kwako, atakufukuzia kwa njia ambayo atakuonyesha ya kuwa anataka kuwa na
mahusiano marefu na wewe. Atakupigia simu mara kwa mara, ataplan jinsi
ya kuspend muda mkiwa pamoja na hatokuacha ukibahatisha hisia ambazo
anazo kwa moyo wake kukuhusu.
Mwanaume ambaye hajajitolea ni yule ambaye hana mpango wala mikakati
yeyote ile. Deti zake anazozipanga zinaonekana kawaida tu na haonyeshi
dalili zozote zile za kuwa anakuthamini.
Kumalizia ni kuwa ukiona mwanaume yeyote ambaye ana dalili zozote ambazo
tumeziashiria hapa, basi fahamu ya kuwa hakutakii mema. Lakini dalili
hizi si kuwa kila mwanaume atamaanisha ya kuwa hajajitolea katika
mahusuano bali labda itakuwa hakujua kama majukumu yalikuwa yanahitajika
baada ya deti.

No comments:
Post a Comment